Home / Michezo / Lukaku akana kuwapigia kelele majirani zake Marekani

Lukaku akana kuwapigia kelele majirani zake Marekani

Lukaku akabiliwa na shtaka la kupigia kelele majirani zake huko Marekani
Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amekana makosa ya kupiga kelele katika nyumba aliyokuwa akiishi baada ya kukamatwa nchini Marekani mapema mwaka huu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alishtakiwa kwa makosa hayo mnamo mwezi Julai baada ya maafisa wa polisi kupata malalamishi mengine matano ya kelele katika nyumba moja ya Beverly Hills.
Raia huyo wa Ubelgiji hakuwasili mahakamani mjini Los Angeles siku ya Jumatatu.
Wakili wake Robert Humphreys aliwasilisha ombi la kutokuwa na makosa hayo.
Kamishna Jane Godfrey aliahirisha kesi hiyo.
Baada ya kusikilizwa, wakili James Eckart alisema kuwa iwapo atapatikana na hatia, mshambuliaji huyo atakabiliwa na faini na kulipa fedha za gharama za simu zilizopigwa kwa siku tano.
Lukaku anaweza kutowasili mahakamani yeye binafsi na badala yake anaweza kutumia wakili wake kumwakilisha.
Maafisa wa polisi wanasema walitoa tamko la onyo baada ya kupata wito kutoka kwa nyumba moja.
Kisa hicho kilitokea wiki moja kabla ya Lukaku kujiunga na Manchester United kutoka Everton kwa kitita cha £75m.
Taarifa ya Beverly Hills wakati huohuo inasema kuwa Lukaku, ambaye alikuwa katika likizo Marekani ,aliwachiliwa katika eneo hilo kufuatia kisa hicho mnamo tarehe 2 mwezi Julai.
Amefunga mabao 11 katika mechi 10 za United.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *