Home / Habari za Kimataifa / Mkuu wa polisi wa Catalonia afikisha mahakamani Uhispania

Mkuu wa polisi wa Catalonia afikisha mahakamani Uhispania

Kamanda Trapero: Polisi wa Mossos walisifiwa kwa kukabiliana na magaidi Barcelona
Mkuu wa polisi katika jimbo la Uhispania la Catalonia, nchini Uhispania Josep Lluis Trapero, amefika mahakama mjini Madrid kama mshukiwa katika uchunguzi kuhusiana na madai ya kuchochea uasi dhidi ya taifa.
Vikosi vyake vimekuwa vikishutumiwa kushindwa kulinda polisi wa taifa dhidi ya waandamanaji kabla ya kura ya maoni yenye utata juu ya uhuru kufanyika.
Afisa mwingine wa polisi wa Catalonia na wanaharakati wawili wa uhuru watahojiwa kama washukiwa.
Mzozo wa kisiasa juu ya azma ya Catalonia ya kutaka kuwa huru umewaacha maafisa wa polisi katika jimbo hilo katika hali ngumu.
Maafisa wamejipata njia panda katika kuamua juu ya utekelezaji wa wajibu wao wa kikazi wa kulinda sheria na huruma kwa wanaotaka kujitenga kwa jimbo Catalonia na Uhispania.
Wengi walichagua kutotekeleza maagizo ya kusitisha kura ya maoni ya uhuru siku ya Jumapili na kuliachia jukumu la kukabiliana na waandamanaji jeshi la polisi la serikali kuu ya Uhispania.

Maandamano ya kuunga mkono uhuru yameendelea hata baada ya kura kufanyika Jumapili

Trapero (pili kutoka kushoto) akiwasili mahakamani Madrid akiwa na wenzake wa Mossos

Mwandamanaji anayeunga mkono uhuru wa Catalonia akiwa karibu na mji wa Barcelona
Kesi hizi zina uhusiano na tukio jingine la awali ambapo maafisa wa polisi walikwama miongoni mwa waandamanaji waliokuwa na hasira wakati wa uvamizi wa majengo ya serikali ya Catalonia.
Catalonia kujitangazia uhuru karibuni
Kamanda wa polisi wa Catalonia, Josep Lluis Trapero, alisifiwa kwa namna alivyoshughulikia shambulio la kigaidi la Barcelona.
Lakini sasa anakabiliwa na maswali kama mshukiwa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *