Home / Habari Za Kitaifa / Mama lishe wakimbiwa ujenzi wa reli

Mama lishe wakimbiwa ujenzi wa reli

BAADHI ya baba na mama lishe wamelalamikia utaratibu uliowekwa na kampuni ya ujenzi wa Reli ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, kwa kuwakataza kufanya biashara hiyo na kumuweka mtu binafsi kuwapa chakula wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Watoa huduma hao walilalamika kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo ambaye alifanya ziara kutembelea eneo la mradi huo ulioko kwenye Kijiji cha Soga wilayani Kibaha.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Moses Mgao alisema walifuata taratibu zote kutoka kwenye kijiji na halmashauri ambao waliwaambia waboreshe kwanza mazingira ikiwa ni pamoja na kujenga choo, mambo ambayo waliyafanya lakini wanashangaa kutakiwa waondoke na wasifanye biashara hiyo.

Kwa upande wake Rukia Ally alisema wametumia gharama kubwa kujenga mabanda wanayofanyia biashara hiyo ya chakula na wamekopa mikopo kwenye taasisi za kifedha hali ambayo inawapa wasiwasi huenda wakauziwa mali zao.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *