Home / Habari Za Kitaifa / Wawekezaji ‘wagombania’ kuendesha kiwanda cha nyama

Wawekezaji ‘wagombania’ kuendesha kiwanda cha nyama

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack amesema wawekezaji kadhaa wamejitokeza kutaka kupewa uendeshaji wa kiwanda cha nyama kilichopo maeneo ya Old Shinyanga, ambacho ni moja ya fursa muhimu za uwekezaji mkoani kwake zilizolala.

Akizungumza na waandishi wa habari, saa kadhaa baada ya kumalizika kwa Jukwaa la Fursa za Biashara lililofanyika Shinyanga, Mkuu wa Mkoa alisema hata hivyo kwamba maombi yamekuwa yakitumwa kupitia Wizara ya Fedha. Alisema mkoa wake sasa umekuwa ukisubiri kupokea maelekezo ya kushirikiana na mwekezaji atakayekuwa na sifa ya kuendesha kiwanda hicho.

Jukwaa la Biashara Shinyanga lililofanyika Alhamisi iliyopita, liliandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha gazeti hili, Daily News na SpotiLeo kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa mkoa alisema baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, aliagiza kiwanda hicho cha nyama kirejeshwe serikalini, jambo ambalo limeshatekelezwa. Alisema mwekezaji mwenye uwezo akipatikana, hatua ya usafirishaji mifugo kutoka Shinyanga kwenda Dar es Salaam itapungua na kwamba ngozi itakayopatikana itakuwa ni zao lingine kwa maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *