Home / Habari za Kimataifa / Hispania yakataa tangazo la uhuru la Catalonia

Hispania yakataa tangazo la uhuru la Catalonia

Wale wanaounga mkono uhuru walikusanyika Barcelona

Serikali ya Hispania imekataa tangazo la kujitangazia uhuru lililotiwa sahihi na kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont na kutupilia mbali wito wa kutaka kuwepo mazungumzo.

Naibu waziri mkuu wa Hispania amemtaja Bw Puigdemont kama “mtu asiyejua yuko wapi au kile anachokifanya”.

Waziri mkuu Mariano Rajoy, anafanya mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kuzungumzia hatua ambazo serikali itachukua.

Hispania yakataa wito wa Catalonia
Polisi watumwa kabla ya hotuba kuu Catalonia

Mr Puigdemont alitia sahihi tangazo la uhuru siku ya Jumanne, lakini akazuia kutekelezwa kwake ili kutoa nafasi kwa mazungunzo.

Kumekuwa na uvumi kuwa rais huyo wa Catalonia anaweza kutangaza uhuru na kutekeleza hatu hiyo yake ambayo itaiweka Hispania katika hali ngumu kisiasa

Hotuba ya Puigdemont

Hispania imekuwa katika hali ya sintofanya tangu kura ya maoni iliyokumbwa na utata Oktoba mosi, ambayo ilitangazwa kuwa isiyo halali na mahaka ya katiba ya nchi hiyo.

Akihutubia bunge la Catalonia mjini Barcelona siku ya Jumanne, Bw Puigdemont alisema kuwa ene hilo linalojitawal,a lilipata haki ya kuwa huru kutokana na kura hiyo.

Rais wa Catalonia asaini kujitenga
Karibu tani 4 za cocaine zakamatwa Hispania

“Tunatoa wito kwa mataifa ya nje na mashirika kutambua taifa la Catalonia kama tafa huru,” alisema.

Yeye na viongozi wengine wa Catalonia kisha wakatia sahihi tangazo la uhuru. Haifahamiki ikiwa tangazo hilo limeambatana na sheria.

Umati unaouga mkono Uhuru mjini Barcelona ulisherehekea matashi yake Bw. Puigdemont, lakini wengi wakaelezea kughadhabishwa wakati alielezea kwa kina msimamo wake.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *