Home / Habari za Kimataifa / Majeruhi wa shambulizi la Mogadishu wasafirishwa Uturuki kwa matibabu

Majeruhi wa shambulizi la Mogadishu wasafirishwa Uturuki kwa matibabu

Majeruhi wa shambulizi la Mogadishu wakifirishwa Uturuki kwa matibabu

Takriban watu 30 wamesafirishwa kwenda nchini Uturuki kupata matibabu ya dharura, kufuatia shambulizi la bomu la siku ya Jumamosi lililotegwa ndani ya lori kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Zaidi ya watu 300 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa kufuatia shambulizi hilo.

Watalii kutoka China watembelea Mogadishu

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika kwenye shambulizi hilo.

Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007.

Zaidi ya watu 300 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa kufuatia shambulizi hilo

Rais Mohamed Abdullahi “Farmajo” Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili.

Mkimbizi kutoka Somalia ateuliwa waziri Canada
Uwanja wa ndege washambuliwa Mogadishu

Reuters walimnukuu Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana.

Anasema kuwa miili mingine ilizikwa na jamaa zao.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *