Home / Habari Za Kitaifa / Wadakwa na kilo 100 za bangi wakiipeleka Dar

Wadakwa na kilo 100 za bangi wakiipeleka Dar

JESHI la polisi mkoani Tabora linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na bangi kiasi cha kilo 100 kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana kamanda wa polisi mkoani Tabora, Wilbrod Mutafungwa alisema kwamba bangi hiyo ilikamatwa kwenye basi la Dar Lux lenye namba za usajili T 332 DGC aina ya HIGHER linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam.

Alisema kwamba jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wananchi wema kwamba kwenye basi hilo kulikuwa na mabegi sita yote yakiwa yamebeba kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya bangi.

Kamanda huyo wa polisi alisema kwamba mara baada ya basi hilo kuwasili wilaya ya Nzega majira ya saa kumi jioni na baada ya kufanya upekuzi ndani ya buti za gari walikuta kiasi hicho cha bangi kikiwa kwenye mabegi sita.

Aliwataja waliokamatwa na bangi hiyo kuwa ni madereva wa gari hilo, Philipo Musa (35) na Said Ngozo (43) wote ni wakazi wa mkoani Iringa na kuongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya jeshi hilo kukamilisha upelelezi wa shauri hilo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *