Home / Habari Za Kitaifa / Atupwa jela miaka 20 kwa shambulio la aibu

Atupwa jela miaka 20 kwa shambulio la aibu

MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imemhukumu Mtandi Nassoro (24), mkazi wa Igunga mjini kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la shambulio la aibu kwa mtoto wa miaka tano, ambaye jina lake limehifadhiwa.

Baada ya kutoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi, Ajali Milazi alisema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri, umethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa mshitakiwa, Mtandi Nassoro, alitenda kosa na hivyo anahukumiwa kwenda jela miaka 20 ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Milazi alisema kwamba tabia ya kuwadhalilisha watoto wa kike, imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hivyo adhabu kali ndio dawa ya kukomesha vitendo vya aina hiyo.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliiambia mahakama kuwa Nassoro alitenda kosa hilo Mei 18 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi katika mtaa wa Stoo mjini Igunga, ambapo alimfanyia shambulio la aibu kwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka tano kwa kumvua nguo za ndani na kumshikashika sehemu za siri.

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri ulipeleka mashahidi watano mahakamani, akiwemo mtoto aliyeshambuliwa, ambao wote walitoa ushahidi wa kumtambua mshitakiwa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *