Home / Habari za Kimataifa / Trump kutoa faili za mauaji ya rais wa zamani John F Kennedy

Trump kutoa faili za mauaji ya rais wa zamani John F Kennedy

Rais Donald Trump amesema kuwa anapanga kuruhusu kufunguliwa kwa faili kuhusu mauaji ya aliyekuwa rais wa Marekani John F Kennedy.
Rais Donald Trump amesema kuwa anapanga kuruhusu kufunguliwa kwa faili kuhusu mauaji ya aliyekuwa rais wa Marekani John F Kennedy.
Rais huyo alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisema ataruhusu kutolewa kwa faili hizo huku wakiendelea kupata habari zaidi.
Faili hizo zinatarajiwa kufunguliwa na makavazi ya Marekani tarehe 26 Oktoba , lakini rais ana uwezo wa kuendelea kuoanisha faili hizo katika makavazi hayo.
Kennedy alipigwa risasi na mtu asiyejulikana mnamo mwezi Novemba 1963 mjini Dalls Texas.

Rais Kennedy akimlalia mkewe baada ya kupigwa risasi
Makavazi ya kitaifa tayari yametoa stakhabadi kadhaa zinazohusiana na mauaji hayo, lakini nakala za mwisho bado hazijatolewa.
”Mbali na kusubiri habari zaidi , mimi kama rais nitaruhusu faili zilizozuiliwa kwa muda mrefu za mauaji ya Kennedy kufunguliwa” , Trump alichapisha ujumbe wa Twitter.
Bunge la wawakilishi nchini humo liliamuru 1992 kwamba stakhabadhi zote za mauaji ya JFK zinafaa kutolewa katika kipindi cha miaka 25 , hadi pale rais aliyepo madarakani atakapodhania kwamba kutolewa kwake kunaweza kukaathiri usalama wa taifa.
Makavazi hayo yana takriban faili 3,000 ambazo haziojatolewa na zaidi ya faili nyengine 30,000 ambazo zilitolewa lakini baada ya fanyiwa uhariri.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *