Home / Habari za Kimataifa / Tundu Lissu asimama kwa mara ya kwanza

Tundu Lissu asimama kwa mara ya kwanza

Tundu Lissu asimama kwa mara ya kwanza akiwa hospitalini Nairobi
Mwanasheria mkuu wa chama upinzani Chadema nchini Tanzania Tundu Lissu, ameweza kusimama kwa mara ya kwanza baada ya kushambuliwa.

Tundu Lissu amekuwa akipokea matibabu Nairobi tangu alipopigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwezi Septemba.

Katika picha iliowekwa katika ukurasa wa Facebook wa CHADEMA, mbunge huyo anaonekena akisimama akisaidiwa na wahudumu wawili wa hospitali.

Ujumbe ulioambatana na picha ukisema “Wiki iliyopita niliwataarifu kwamba madaktari wangu wamesema ‘nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania.Leo Boxing Day (Tarehe 26 Disemba) nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa ‘Mababa Cheza’ wangu. Hatua inayofuata ni magongo kesho na nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu.”

Makamu wa rais wa Tanzania amtembelea Tundu Lissu
Tundu Lissu: Kushambuliwa kwangu kulichochewa na siasa Tanzania
Bwana Lissu ambaye pia ni mkuu wa chama cha mawakili nchini Tanzania amekuwa akizozana na serikali ya Rais Magufuli na alikamatwa mara sita mwaka huu pekee, akishtumiwa kwa kumtusi kiongozi huyo wa taifa mbali kuharibu usalama wa umma, miongoni mwa mashtaka mengine.amesema anaamini kushambuliwa kwake kulihusiana na siasa nchini humo.

Akizungumza na BBC hivi karibuni mbunge huyo wa Singida Mashariki amelilaumu Bunge la nchi hiyo akisema halijachukua hatua zozote kumsaidia tangu kulazwa kwake hospitalini.

Makamu wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu alimtembele

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *