Home / Habari za Kimataifa / Aliyemuondoa madarakani Mugabe ateuliwa makamu wa rais

Aliyemuondoa madarakani Mugabe ateuliwa makamu wa rais

Jenerali wa zamani wa Jeshi Constantin Chiwenga ateuliwa kuwa makamu wa rais wa Zimbabwe
Aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini Zimbabwe Constantin Chiwenga ameteuliwa kuwa makamu mpya wa rais wa Zimbabwe.

Bwana Chiwenga aliongoza jeshi kumtimua mamlakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Robert Mugabe mnamo mwezi Novemba.

Alistaafu hivi majuzi na kuwa naibu wa chama tawala cha Zanu-Pf mnamo Disemba 23.

Naibu mwengine wa chama tawala cha Zanu-Pf ,aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Zimbabwe Kembo Mohadi pia atateuliwa kuwa makamu wa rais.

Jenerali Chiwenga aliyechukua mamlaka ya Mugabe
Jenerali wa jeshi aliyemng’oa Mugabe sasa ni naibu wa Zanu-PF
Rais Mugabe amtunuku shahada mke wa Jenerali aliyemzuia
Rais mpya Emmerson Mnangagwa alichukua mamlaka baada ya jeshi kuingilia kati mnamo tarehe 15 mwezi Novemba kufuatia mgogoro wa kumrithi Robert Mugabe.

Siku chache kabla ya jeshi kuchukua mamlaka , bwana Mnangagwa , wakati huo akiwa naibu wa rais alifutwa kazi na kuondoka nchini humo katika kile kilichoeleweka kuwa jaribio la rais kumpatia uongozi mkewe Grace kuwa mrithi wake.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mtanzania mwanaharakati Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Rebeca Gyumi Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *