Home / Michezo / Mbao FC yapeleka kilio Jangwani ikiifunga mabao 2-0

Mbao FC yapeleka kilio Jangwani ikiifunga mabao 2-0

Mbao FC imewafunga mabingwa watetezi Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu baada ya kuifunga mabao 2-0.

Mwanza. Kikosi cha Mbao FC kimeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Yanga mabao yaliyofungwa na Habibu Haji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Mabao hayo ya Mbao FC yameishusha Yanga hadi nafasi ya nne ikibaki na pointi 21 huku Singida United wakisogea nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 23 baada ya kuifunga Njombe Mji kwa mabao 3-1.

Ushindi wa Mbao umekuwa kaa la moto kwa Yanga baada ya kufunga mwaka leo Jumapili kwa kupoteza mchezo huo wa Ligi Kuu.

Wakati Yanga wakikutana na balaa hilo, watani zao Simba wamefanikiwa kujiweka kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC mchezo uliopigwa jana Jumamosi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *