Home / Habari za Kimataifa / Msichana mpalestina aliyerekodiwa akiwapiga wanajeshi wa Israel ashtakiwa

Msichana mpalestina aliyerekodiwa akiwapiga wanajeshi wa Israel ashtakiwa

Ahed Tamimi, 17, na binamu yake walirekodiwa kwenye video wakiwakabili wanajeshi wa Israel
Mamlaka za Israel zimemfungulia mashtaka msichana mpalestina ambaye alirekodiwa kwenye video akimshambulia mwanajeshi wa Israel.

Ahed Tamimi, 17, na binamu yake walirekodiwa kwenye video wakiwakabili wanajeshi wa Israel katika kanda iliyosambaa pakubwa katika mitandao ya kijamii.

Anakabiliwa na kesi 12 ikiwemo dhuluma na kurusha mawe.

Lakini familia yake inasema kuwa walihusika kwenye maandamano katika eneo linalokaliwa na Israel la Ukingo wa Magharibi.

Wapalestina wamuita balozi wao kutoka Marekani
Mwanajeshi wa Israel miezi 18 jela kwa kumuua Mpalestina
Jerusalem: Mataifa ya kiarabu yalaani hatua ya Marekani
Jeshi la Israel linasema kuwa wanajeshi hao walikuwa wakiwazuia wapalestina kutokana na kurusha mawe kwa waendesha magari.

Video hiyo iyorekodiwa tarehe 15 Disemba ilionyesha kikundi cha wanawake akiwemo Tamini, wakiwapiga wanajeshi wawili wa Israel waliokuwa wamejihami vikali.

Ilisambaa sana katika mitandao na wapalestina wengi wamemsifu Tamini kuwa shujaa kwa kuipinga Israel.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *