Home / Habari Za Kitaifa / Rais John Magufuli awalilia 36 waliokufa ajalini Kenya

Rais John Magufuli awalilia 36 waliokufa ajalini Kenya

WAKATI Serikali ya Kenya ikipiga marufuku mabasi ya abiria kusafi ri usiku kutokana na ajali ya lori na basi, iliyosababisha vifo vya watu 36 na kujeruhi watu kadhaa mwishoni mwa wiki, Rais John Magufuli ameungana na Wakenya kuomboleza vifo hivyo.

Ametuma salamu za rambirambi kwa Rais Uhuru Kenyatta, akimweleza ameguswa na kushitushwa na taarifa za ajali hiyo, aliyosema imesababisha majonzi si kwa Wakenya pekee, bali nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa ujumla.

Katika taarifa yake iliyotelewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli alisema; “Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa ajali iliyosababisha ndugu zetu takribani 36 kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana na roli katika barabara ya Nakuru – Eldoret nchini Kenya.

“Msiba huu umesababisha majonzi makubwa siyo tu kwa ndugu zetu wa Kenya bali pia kwetu sote wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumepoteza wapendwa wetu na nguvu kazi yetu.

“Kwa niaba ya Watanzania wote nakupa pole sana ndugu yangu Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa msiba huu mkubwa ulioupata, nawapa pole wana familia wote waliowapoteza jamaa zao na pia nawapa pole wananchi wote wa Kenya.

“Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, nawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapone haraka na Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina”. Kutokana na ajali hiyo, Kenya imeungana na Tanzania kufuta safari za usiku kwa mabasi ya abiria, lengo likiwa kudhibiti ajali ambazo kwa kiasi kikubwa zimeonekana kutokea nyakati za usiku.

Uamuzi huo wa Kenya ulitangazwa juzi na Mamlaka ya Usafiri na Usalama (NTSA) kupitia Mkurugenzi wake, Francis Meja ikiwa ni siku moja baada ya kutokea kwa ajali ya basi kugongana uso kwa uso na lori na kusababisha vifo vya watu 36. Tanzania ilichukua uamuzi huo zaidi ya miaka kumi iliyopita. Na kutokana na agizo jipya, safari za mabasi Kenya sasa zitafanyika kati ya saa 12 asubuhi na saa moja usiku

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

CCM YASHINDA UBUNGE, UDIWANI KWA 100%

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshinda kwa asilimia 100 kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Buyungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *