Home / Michezo / Everton kumchukua mshambuliaji wa Besiktas Cenk Tosun kwa £27m

Everton kumchukua mshambuliaji wa Besiktas Cenk Tosun kwa £27m

Everton wamekubaliana na klabu ya Besiktas ya Uturuki kuhusu kumnunua mshambuliaji Cenk Tosun.

Meneja wa Everton Sam Allardyce amesema kilichosalia sasa ni makubaliano kati ya klabu na mchezaji huyo.

Everton walifanya mkutano na rais wa Besiktas Fikret Orman Jumatano kuhusu uhamisho ambao unatarajiwa kuwa wa £27m.

Tosun, 26, amekuwa London akisubiri idhini ya kukamilisha uhamisho huo.

Allardyce amesema anatumai Tosun atasajiliwa kwa wakati kumuwezesha kucheza dhidi ya Liverpool katika raundi ya tatu ya Kombe la FA Ijumaa.

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 04.01.2018
Tosun aliwasaidia Besiktas kufika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ambapo watakutana na Bayern Munich.

Allardyce anatarajia mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uturuki ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani atazalisha magoli Everton baada ya klabu hiyo kukaukiwa na mabao baada ya Romelu Lukaku kuhamia Manchester United kwa £90m.

Tosun ndiye mchezaji wa kwanza kununuliwa na Allardyce tangu kuondoka kwa Ronald Koeman.

Cenk Tosun amefunga mabao manane mechi 24 alizochezea Uturuki

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *