Home / Habari za Kimataifa / Vikosi vya Syria vyashambulia hospitali maeneo ya waasi Syria

Vikosi vya Syria vyashambulia hospitali maeneo ya waasi Syria

Majengo yameharibiwa vibaya na mapigano hayo yanayoendelea
Wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Syria wanasema kwa siku kumi mfululizo,vikosi vya serikali ya Syria vimekuwa vikishambulia hospitali katika maeneo yanayokaliwa na waasi nchini humo.

Mshauri wa masuala ya afya wa Umoja wa Mataifa aliyepo nchini humo Hamish de Bretton-Gordon amesema mashambulizi hayo yanarudisha nyuma juhudi zao za kuwapatia watu huduma za afya.

Anasema hospitali zimeharibiwa vibaya Mashariki mwa mji wa Ghouta na Damascus,na jimbo la Kaskazini la Idlib.

Bretton-Gordon amesema zaidi ya watoto 150 wanahitaji kuondolewa katika maeneo hayo ili kupata huduma kamili za afya.

Hali ya usalama nchini Syria imekua ya kuzorota kila kukicha kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya serikali na washirika wake dhidi ya waasi wanaopinga serikali ya Rais Bashar al-Assad.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *