Home / Michezo / Man City wana ‘kikosi ghali zaidi katika’ soka duniani

Man City wana ‘kikosi ghali zaidi katika’ soka duniani

Manchester City ndiyo klabu iliyo na wachezaji ghali zaidi duniani kwa pamoja, kwa mujibu wa utafiti wa shirika la CIES Football Observatory.

City walitumia £215m dirisha la kuhama wachezaji katika majira ya joto na kufikisha jumla ya gharama ya kikosi chao hadi euro 853m (£775m).

Thamani hiyo ni £3m zaidi ya pesa zilizotumiwa na Paris St-Germain, waliomnunua Neymar majira ya joto kwa rekodi ya dunia ya £200m.

Manchester United, ambao wametumia euro 784m (£712m) kuunda kikosi chao cha sasa, wanashikilia nafasi ya tatu.

Walikuwa wanaongoza mwaka uliopita, lakini thamani ya kikosi chao ilipanda kwa £66m pekee majira ya joto.

Klabu za England zilivyovunja rekodi kuwanunua wachezaji
Takwimu za CIES zinaangazia ligi tano kuu za Ulaya – ligi kuu za England, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania.

Klabu za Ligi ya Premia zinajaza nafasi sita kati ya nafasi kumi za juu, ambapo vikosi vyake vina thamani ya wastani ya euro 287m (£261m).

Vikosi ghali zaidi
Klabu Nchi Gharama (euro)
Manchester City England 853
Paris St-Germain Ufaransa 850
Manchester United England 784
Chelsea England 644
Barcelona Uhispania 628
Real Madrid Uhispania 497
Juventus Italia 470
Liverpool England 437
Arsenal England 416
Tottenham England 361

machester city. habari za michezo

Chanzo: www.bbc.com/swahili

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *