Home / Michezo / Yanga hesabu zimekubali

Yanga hesabu zimekubali

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Yanga jana walitoka sare ya bao 1-1 na St Louis ya Shelisheli kwenye mechi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na kusonga mbele.

Yanga imesonga mbele kwa mabao 2-1 baada ya kushinda bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam.

Ikiwa ugenini Victoria jana, Yanga ilitawala karibu muda wote wa mchezo huo kabla wenyeji hawajazinduka dakika za mwisho za kipindi cha pili na kusawazisha bao.

Ibrahim Ajibu ndiye aliyeifungia Yanga bao jana katika dakika ya 45 baada ya kupata krosi nzuri ya Hassan Kessy.

Kwa ushindi huo Yanga inatarajiwa kukutana na mshindi kati ya El Mereikh ya Sudan au Township Rollers ya Botswana waliotarajiwa kucheza jana usiku.

Katika mechi ya kwanza Merreikh ilifungwa mabao 3-0 ugenini Botswana. Yanga licha ya kucheza bila mshambuliaji wake tegemeo, Obrey Chirwa jana ilicheza vizuri na kwa kujiamini ingawa ilishindwa kutumia nafasi kadhaa ilizopata.

Dakika ya sita tu kuanza kwa mchezo huo Papy Tshishimbi alipata nafasi ya wazi ikapanguliwa na kipa wa Louis, pia, dakika 23 alipata nafasi akapaisha mpira nje.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Willian anasema hakuna sababu ingemfanya kusalia Chelsea iwapo Antonio Conte angebakia

Willian alifunga magoli 13 na kutoa pasi 12za usaidizi katika mechi 55 za Chelsea msimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *