Home / Habari za Kimataifa / Watu Wote: Filamu ya Kenya yakosa kushinda Tuzo ya Oscar 2018

Watu Wote: Filamu ya Kenya yakosa kushinda Tuzo ya Oscar 2018

Filamu kuhusu shambulizi la kigaidi la al-Shabab nchini Kenya ambayo ilisifiwa sana baada ya kushinda tuzo ya Oscars kitengo cha wanafunzi mwaka jana, haikufanikiwa kushinda tuzo kuu katika Tuzo za Oscars.

Filamu hiyo kwa jina Watu Wote inahusu shambulio ambapo watu 2 waliuawa ndani ya basi eneo la Mandera mwaka 2015.

Watu Wote ilikuwa imeteuliwa kushindania tuzo ya Oscar katika kitengo cha Filamu Fupi kuhusu Matukio Halisi lakini washindi wa tuzo walipotangazwa, ikabwagwa na filamu ya The Silent Child ambayo waigizaji wake nyota Rachel Shenton na Chris Overton wanatokea Uingereza.

Filamu ya The Silent Child inaangazia maisha ya msichana wa miaka minne asiyeweza kusikia anayeishi maeneo ya mashambani England.

Shenton alitoa hotuba yake ya kupokea tuzo kwa lugha ya ishara ambapo alisema: “Nilitoa ahadi hii kwa mwigizaji wetu nyota ambaye ana miaka sita kwamba ningetoa hotuba hii kwa lugha ya ishara. Mikono yangu inatetemeka, kwa hivyo naomba radhi,” alisema.
“Filamu yetu inahusu mtoto asiyeweza kusikia ambaye anazaliwa katika ulimwengu wa kimya. Si filamu iliyoongezwa chumvi, haya ni mambo ambayo yanawatendekea mamilioni ya watoto kote duniani ambao huishi katika kimya na kukumbana na matatizo katika kuwasiliana na hasa katika kupata elimu.”

Kwa Picha: Tuzo za Oscars mwaka 2018
Waislamu waokoa wakristo waliotekwa na Alshabab
Wakristo na Waislamu waonyesha umoja Kibera Kenya
“Kutoweza kusikia ni ulemavu wa kimya, ninataka kutoa shukrani zangu kwa watoaji wa tuzo hizi kwa kutuwezesha kueleza hili kwa watu wengi.”

Licha ya kukosa kushinda, Wakenya wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta wamekuwa wakiwapongeza walioshiriki katika kuigiza filamu hiyo ya Watu Wote wakiwapa heko kwa kazi nzuri.

Wanafunzi Wakenya kutoka taasisi ya filamu ya Africa Digital Media Institute (ADMI) walishiriki katika kuigiza filamu hiyo wakishirikiana na wanafunzi kutoka Ujerumani
Hotuba kwa lugha ya ishara
Overton – ambaye anachumbiana na Shenton – alikuwa mwelekezi wa filamu hiyo. Nafasi ya msichana huyo mlemavu kwa jina Libby iliigizwa na Maisie Sly ambaye pia ana tatizo la kusikia.

Shenton ni mmoja tu miongoni mwa waigizaji wachache wa kike kuwahi kutoa hotuba kwa lugha ya ishara. Jane Fonda alitoa sehemu ya hotuba yake ya ushindi kwa lugha ya ishara kwa filamu yake ya

Coming Home mwaka 1979. Louise Fletcher pia alitoa hotuba kwa lugha ya ishara kwa sababu ya wazazi wake wasioweza kusikia aliposhinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike kwa filamu yake ya One Flew Over The Cuckoo’s Nest miaka mitatu awali.

Marlee Matlin, ambaye ana matatizo ya kusikia, pia alitoa hotuba kwa lugha ya ishara baada ya kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike kwa filamu yake ya Children Of A Lesser God mwaka 1987.

Watu Wote ndiyo filamu ya kwanza kutoka Kenya kushinda tuzo za Oscars kitengo cha wanafunzi.

Filamu hiyo inayoeleza hadithi ya Kenya, kuhusu Wakenya na inashirikisha waigizaji wa Kenya, inasimulia shambulio hilo la mwaka 2014 kaskazini mwa Kenya, ambapo maudhui ya uadui wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu unaangaziwa.

Filamu ya Kenya yashinda tuzo ya Oscars
Lupita Nyong’o ndiye Mkenya pekee kuwahi kushinda tuzo ya Oscar kufikia sasa, aliposhinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike msaidizi kwa uigizaji wake katika filamu ya 12 Years a Slave mwaka 2014.

Filamu hiyo inaangazia jinsi Waislamu waliwakinga Wakristo wakati wa shambulio la kigaidi

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda baada ya dereva wake kuuawa

  Boni Wine Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *