Home / Habari za Kimataifa / Mwanamume aliyepasuliwa ubongo kimakosa Kenya azungumza

Mwanamume aliyepasuliwa ubongo kimakosa Kenya azungumza

Mwanamume aliyepasuliwa ubongo kimakosa Kenya azungumza
Mwanamume ambaye alifanyiwa upasuaji wa ubongo kimakosa nchini Kenya ameruhusiwa kuondoka hospitalini na kuzungumzia masaibu yaliyompata

Akiwa na alama kubwa kichwani, Samwel Kimani aliiambia televisheni ya NTV kuwa, alikuwa amepoteza fahamu wakati alilazwa hospitalini na hakufahamua kilichosababisha madaktari kumfanyia upasuaji.

Hospitali ya Kenyatta iliomba msamaha baada ya kukiri kuwa vifaa vya kutambua wagonjwa hao wawili vilikuwa vimechanganyika.

Mgonjwa apasuliwa ubongo kimakosa hospitalini Kenya
Mwanamume ambaye alistahili kufanyiwa upasuaji wa ubongo kufuatia kuganda kwa damu naye aliruhusiwa kurudi nyumbani lakini bado haijulikani ikiwa anahitaji kufanyiwa upasuaji huo.

Kisa hicho kimewashangaza wakenya wengi tangu kiibuke na kilisababisha afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta nchini Kenya kutumwa kwenye likizo ya lazima.

Hatua ya kumtuma Lilly Koros kwenye likizo ya lazima ilitangazwa na Waziri wa afya Sicily Kariuki ambaye alisema hatua hiyo ilikusudiwa “kupisha uchunguzi”.

Wanawake waandamana kuhusu madai ya ubakaji katika hospitali Kenya
Mmoja kati yao wagonjwa hao ndiye alihitaji upasuaji wa kichwa ili kuondoa damu iliyokuwa imeganda kwenye ubongo wake.

Huyo mwingine alikuwa amefura kwenye kichwa lakini alihitaji matibabu ambayo hayakushirikisha upasuaji.

Lakini asiyehitaji upasuaji ndiye aliyeishia kufanyiwa upasuaji. Madaktari waligundua kosa hilo saa chache baada yao kuanza upasuaji walipogundua kwamba hawakuweza kuiona damu iliyoganda kwenye ubongo wa mgonjwa waliokuwa wanamfanyia upasuaji.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *