Home / Michezo / Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.03.2018

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.03.2018


Joachim Low
Kocha wa Ujerumani Joachim Low, mwenye umri wa miaka 58, ndiye anayepigiwa upatu kumrithi Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal iwapo raia huyo wa Ufaransa ataondoka katika klabuhiyo msimu wa joto. (ESPN)

Kuna hisia miongoni mwa wachezaji wa Gunners ya kutopendelewa wanaolipwa mishahara mikubwa katika kalbu hiyo ya ligi ya England. (Times)

Kipa wa Manchester United David de Gea bado anasubiri pendekezo la mkataba mpya licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Uhispania kusalia na miezi 16 katika mkataba aliyonao sasa. (Yahoo)

Ryan Sessegnon (kati kati)
Mchezaji wa Fulham Ryan Sessegnon anapendelea kuhamia Tottenham, lakini mchezaji huyo wa timu ya taifa ya England kwa wachezaji wa chini ya miaka 19 anawaniwa na pande tofuati katika ligi ya England. (mirror)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Everton Dominic Calvert-Lewin, huenda akaitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England wakati Kombe la dunia likitarajiwa msimu huu wa joto. (Mirror)

Ajenti wa mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Emre Can, ‘amezuia majadiliano yote’ kuhusu mustakali wa mchezaji huyo mweny umri wa miaka 24 raia wa Ujerumani. (Express)

Manchester United wanapanga mazungumzo ya mkataba mpya na mchezaji wa kiungo cha mbele mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ufaransa Anthony Martial. (ESPN)

Kaka: Nyota wa zamani wa Brazil na AC Milan astaafu
Timu ya AC Milan yanunuliwa na kampuni ya China
Matumaini ya Liverpool kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Barcelona Ivan Rakitic yameingia dosari huku mabingwa wa La Liga wakiwa na dhamira ya kuendelea kumzuia raia huyo wa Croatia (AS, kupitia Talksport)

Newcastle ndio wanaopigiwa upatu kumsajili mchezaji wa Porto mwenye umri wa miaka 36 ambaye alikuwa kipa wa Uhispania Iker Casillas katika uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Newcastle Chronicle)

Iker Casillas
Brighton, Crystal Palace na West Ham zote zinamuwani mlinzi wa Lille Ibrahim Amadou, mwenye umri wa miaka 24, ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya kimataifa ya vijana Ufaransa. (Le 10 Sport, kupitia Croydon Advertiser)

Kipa wa Liverpool Simon Mignolet yupo tayari kuondoka Anfield huku Napoli na Borussia Dortmund zote zikiwaza kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (DH )

AC Milan wanataka kumsajili mlinzi wa Porto Ivan Marcano wakati mkataba wa Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 30 ukimalizika msimu wa joto.(Calciomercato )

Deulofeu ajiunga na AC Milan
Raundi ya 3 ya EFL
Mlinzi wa Sunderland Michael Ledger, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na timu ya Norway Notodden FK. (Sunderland Echo)

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Margate Jordan Chiedozie, ametimuliwa kwa kumcheka mchezaji wa timu pinzani aliyeanguka katika mechi dhidi ya Leiston. (Kent Live)

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *