Home / Michezo / Mikel Arteta apigiwa upatu kumrithi Arsene Wenger Arsenal

Mikel Arteta apigiwa upatu kumrithi Arsene Wenger Arsenal

Mikel Arteta na mkufunzi mkuu wa Manchester City Pep Guardiola

Naibu mkufunzi wa klabu ya Manchester City Mikel Arteta ni miongoni mwa wakufunzi wanaopigiwa upatu kumrithi mkufunzi wa Arsenal anayeondoka Arsene Wenger.

Raia huyo wa UHispania ambaye aliichezea The Gunners mara 150 alianza kuwa naibu wa kocha katika klabu ya City 2016.

Hakuna makubaliano yalioafikiwa kufikia sasa kuhusu mkufunzi aliyechaguliwa na kwamba klabu hiyo haijakuwa tayari kuajiri kocha mpya.

Hatahivyo klabu hiyo ina matumaini kwamba itamtaja mrithi wa Wenger kabla ya kombe la dunia linaloanza Juni 14.

Uamuzi utakapoafikiwa na afisa mkuu mtendaji Ivan Gazidis , mkuu wa uhusiano wa soka Raul Sanllehi na mkuu wa usajili Sven Mislintat , watatu hao watawasilisha mapendekezo yao kwa bodi ya Arsenal ili wakurugenzi kuidhinisha.

Wenger ataisimamia Arsenal kwa mara ya mwisho siku ya Jumapili dhidi ya Huddersfield baada ya miaka 22 katika uongozi wake.

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique pia amehusishwa na kazi hiyo pamoja na mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri.

Kulingana na mwandishi wa habari za michez wa BBC David Ornstein Allegri ndiye anayepigiw upatu na wchanganuzi lakini Arteta ameorodheshwa na ijapokuwa Arsenal inasema kuwa wawili hao ndio huenda wakachukua wadhfa huo sio wakufunzi pekee walioorodheshwa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *