Home / Habari Za Kitaifa / IFM yazindua programu tatu za mafunzo

IFM yazindua programu tatu za mafunzo

CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimezindua programu tatu za mafunzo zikiwemo shahada mbili za uzamivu katika masuala ya Uhifadhi wa Jamii, Sera na Maendeleo (MSPD) pamoja na nyingine ya Bima na Elimu ya Uhai wa Bima, kikiwa na lengo la kupunguza pengo lililopo katika jamii.

Programu nyingine iliyozinduliwa ni Shahada ya Kwanza ya Bima na Elimu ya Uhai wa Bima, ambazo kwa pamoja zinatajwa kuwa mkombozi katika jamii hususani kwa kuzalisha wataalamu mbalimbali watakaotoa elimu juu ya masuala hayo, na hivyo kutatua changamoto juu ya masuala ya bima iliyopo kwa sasa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hizo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema kuzinduliwa kwa programu hizo kuna umuhimu mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa, na hasa kwa kuongeza ukuaji wa Pato la Taifa (GDP).

Dk Kijaji alisema sekta ya bima kwa kiasi kikubwa haijawa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi ikichangia wastani wa asilimia moja katika Pato la Taifa licha ya umuhimu wake mkubwa, hivyo kwa kupitia kwa programu hizo ni wazi kutasaidia kuleta mabadiliko chanya. Aidha, alisema programu hiyo pia itaenda kusaidia kuzalisha ajira katika jamii kwa wataalamu watakaohitimu kuwa kama chanzo cha watengeneza ajira kwa kada mbalimbali katika sekta zote za uhifadhi wa jamii, sera na maendeleo pamoja na bima.

Awali Mkuu wa IFM, Profesa Tadeo Satta alisema kuanzishwa kwa programu hizo, kulizingatia mahitaji yaliyopo katika jamii hususani elimu juu ya uhifadhi wa jamii na elimu ya ziada katika masuala ya bima, kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa wataalamu wa sekta hizo katika jamii. Alisema kutokana na changamoto hiyo, taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau, walifanya utafiti na kuona haja ya kuanzisha programu hizo kwa lengo la kutatua changamoto iliyokuwepo.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *