Home / Michezo / Mali U-20 hawatoki kwa Ngorongoro

Mali U-20 hawatoki kwa Ngorongoro

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes, leo itakuwa na kibarua kingine kwenye uwanja wa Taifa kukipiga na vijana wenzao wa Mali.

Mechi hiyo ni ya raundi ya pili kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa vijana wa umri huo ambapo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Niger. Ngorongoro imefika hatua hiyo baada ya kuiondosha Congo DR kwa mikwaju ya penalti 6-5. Timu hizo zilipigiana penalti baada ya kutoka suluhu katika mechi zote mbili, Dar es Salaam na Kinshasa. Kocha wa Ngorongoro, Ammy Ninje alisema kikosi chake kina morali kubwa, kwani kinataka kusonga mbele na kufuzu fainali hizo.

Hata hivyo, alikiri kuwa Mali ni timu nzuri ambayo amekuwa akiifuatilia kwa karibu na kuongeza kuwa maandalizi na utayari wa wachezaji wake ndiyo siri itakayoisambaratisha timu hiyo. “Mchezo utakuwa wa ushindani, Mali nimeifuatilia muda mrefu, wengi wa wachezaji wake ni wale waliocheza timu ya vijana chini ya miaka 17, hivyo wachezaji wako vizuri tutafanya vyema wachezaji wakifanya nilichowaagiza,” alisema Ninje.

Kikosi hicho kitakuwa na faida ya kuutumia uwanja wa nyumbani katika mchezo wa raundi ya kwanza na kurejeshwa kwa kipa Ramadhan Kabwili aliyetemwa awali na kocha huyo kwa sababu za kuchelewa mazoezini wakati akiitumikia klabu nyake ya Yanga. Baada ya mchezo huo kutakuwa na mchezo wa marudiano ambao mshindi ataingia raundi ya tatu ambayo ndiyo itakuwa ya mwisho kabla ya kutinga fainali. Kocha huyo anaamini kuwa mashabiki ni sehemu ya mchezo hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo ili kuwaongezea nguvu zaidi.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *