Home / Afya / Je unakula chakula bora kulinda heshima yako nyumbani?

Je unakula chakula bora kulinda heshima yako nyumbani?

WANAUME wana kawaida ya kupenda kufahamika kwa umahiri wao kimwili na matokeo yake hujiita kwa majina mbalimbali. Utawasikia wakijiita rijali, dume, jembe majina mengine mengi.

Hata hivyo, takwimu zinaonesha kuwa asilimia 60, wanaume wanandoa wakiwamo wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa nyakati fulani au katika muda mwingi wa maisha yao. Matokeo yake, mabango ya waganga wa jadi barabarani yakitangaza tiba yamekuwa yakiongezeka, ingawa hayajafanikiwa kupunguza tatizo hilo. Vijana wa umri wa miaka 18 hadi 48 ndiyo wanaoongoza kwa tatizo hili na tatizo lao limekuwa likiongezeka siku hadi siku kutokana na mfumo wa maisha. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amesema utafiti wa kisayansi duniani unaonesha kuwapo kwa tatizo la nguvu za kiume.

Ametaja baadhi ya sababu zinazochangia tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume ni ulaji wa vyakula vya mafuta, kutofanya mazoezi, matumizi ya ulevi wa pombe, na uvutaji sigara na uvaaji wa nguo za kubana. Hata hivyo, kwa mujibu wa mtandao wa www.menshealth.com/ nutrition/ unatoa orodha mbalimbali ya vyakula ambavyo mwanaume anaweza kutumia ili kupata suluhisho la uhakika kwa kuzingatia vyakula vinavyoweza kuongeza stamina na kujenga mwili vizuri na kuupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri bila ya kutumia ‘booster’.

Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili kulinda heshima yako nyumbani? Vitu vinavyoweza kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume ni kama: •Kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume. •Kutokuwa na kiwango cha kutosha cha homoni ya testosterone •Kupungukiwa protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume Kwa mujibu wa mtandao wa www.menshealth.com/nutrition/imetoa baadhi ya vyakula ambavyo vinaweza kusaidia kuboresha nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda mahusiano.

Chocolate Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwa sababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi. Blueberry Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini.

Damu ndiyo kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi. Mtini (Figs) Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndiyo kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume. Karanga/lozi Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini.

Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi. Vitunguu saumu Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi. SPINACHI Kikombe kimoja cha mboga ya majani aina ya spinach kimejaa magnesiamu, madini muhimu kwa miili ya binadamu ambao unafanya mzunguko wa damu kuwa mzuri, mwili kupata nguvu na kuongeza stamina ya kufanya mapenzi. Ndizi Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *