Home / Afya / Saratani ya kizazi yaathiri wanawake 466,000

Saratani ya kizazi yaathiri wanawake 466,000

ZAIDI ya wanawake 466,000 duniani, wengi wao wakiwa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, huathirika na saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka.

Hayo yalibainishwa jana Jijini Dodoma na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Kiologwe wakati akifungua semina ya siku moja kwa wanahabari kuhusu uanzishwaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi mkoani humo. Dk Kiolongwe alisema saratani hiyo ya mlango wa kizazi, inashika nafasi ya pili kwa kusababisha saratani kwa wanawake huku nafasi ya kwanza, ikiwa ni saratani ya matiti. Alisema kutokana na hayo, saratani hizo mbili kwa pamoja husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama, vitokanavyo na saratani nchini.

Akielezea dalili za saratani hiyo, Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa wa Dodoma, Paulo Mageni alibainisha kwamba takribani saratani zote za mlango wa kizazi, husababishwa na virusi viitwavyo Papilloma (HPV) ambapo visababishi vya maambukizi ya virusi hivyo. “Sababu nyingine ni pamoja na kuanza kujamiiana katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuwa na ndoa za mitala, kuzaa watoto wengi pamoja na uvutaji wa sigara,” alisema Mageni.

Aliongeza: “Dalili za saratani ya mlango wa kizazi ni kutokwa damu bila mpangilio au kutokwa damu baada ya kujamiiana, maumivu ya mgongo, miguu na kiuno, kuchoka, kupungua uzito, kutokwa uchafu kwenye uke wa majimaji uliopauka wa rangi ya kahawia au wenye damu, kuvimba mguu mmoja na kupungukiwa hamu ya kula.”

Alisema kuwa Serikali imeamua kutoa chanjo hiyo kwa watoto kuanzia umri wa miaka 9 hadi 14, ambapo huduma hiyo itatolewa katika vituo mbalimbali vya afya na maeneo ya shule na kuwafuata watu majumbani. Alisema kuwa chanjo hiyo kwa kuanza wataanza kuitoa kwa watoto wenye umri wa miaka 14 kwa muda wa miaka miwili na baada ya hapo wataanza kuitoa kwa watoto wa miaka 9 na kuendelea.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *