Home / Habari za Kimataifa / Picha ya Ozil, Gündogan na Erdogan yazusha hasira kubwa Ujerumani

Picha ya Ozil, Gündogan na Erdogan yazusha hasira kubwa Ujerumani

Mesut Özil (kushoto) alimkabidhi rais Erdogan jezi yake ya Arsenal

Shirikisho la soka Ujerumani (DFB) limeshutumu wachezaji wake wa kimataifa Mesut Özil na Ilkay Gündogan kwa kupiga picha na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Wachezaji hao wawili waliozaliwa Ujerumabni, wote wenye asili ya Kituruki, walimkabidhi Erdogan fulana zao walizozisaini katika hafla moja mjini London siku ya Jumapili.

Gündogan aliandika: “kwa mtukufu rais wangu, kwa heshima kubwa.” Erdogan anafanya kampeni ya kutaka kuchaguliwa upya kama rais Uturuki.

Özil anaichezea timu ya Arsenal na Gündogan anaichezea Manchester City.

Woote wawili wanajitayarisha kwa kombe la dunia mwezi ujao nchini Urusi, ambapo Ujerumani ni miongoni mwa timu zinaozpigiwa upatu ushinda. Uturuki haikufuzu.

Nyota watatu wa Uturuki walipiga picha na bwana Erdogan (kutoka kushoto): Ilkay Gündogan (Man City); Mesut Özil (Arsenal) na Cenk Tosun (Everton)

Wansiasa wengi Ujerumani wamewashutumu wachezaji hao wa soka, wakihoji uadilifu wao kwa maadili ya demokrasia ya Ujerumani.

Rais wa shirikisho hilo la soka Ujerumani DFB Reinhard Grindel amesema: “Soka na DFB zinalinda maadili ambayo hayaheshimiwa vya kutosha na Bwana Erdogan.

“Ndiyo sababu sio vizuri kwa wachezaji wetu wa kimataifa wakubali kuhadaiwa na kampeni yake ya uchaguzi. Kwa kufanya hivyo, wachezaji wetu hawajasaidia jitihada za DFB katika kushughulikia utangamano.”

Mkurugenzi wa DFB Oliver Bierhoff amesema: “hakuna kati yao aliyetambuwa ujumbe unaotokana na picha hiyo, lakini ni wazi kwamba ni makosa na tuazungumza nao kuhusu hilo”.

Katika ujana wake, kabla ya kuingia katika siasa katika miaka ya 90, Erdogan aliichezea timu ya Istanbul, Kasimpasa.

Erdogan, ambaye amehudumu kama kiongozi wa Uturuki kwa miaka 15 sasa anatafuta kuchaguliwa tena katika uchaguziw a dharura Juni 24.

Rais Erdogan na mkewe

Baada ya shutuma hizo kuzuka, Gündogan ametoa taarifa akijitetea, pamoja na wachezaji Özil na Cenk Tosun kuhusu kukutana na Erdogan.

Walikutana kando kando mwa hafla moja kwenye taasisi ya Uturuki inayowasaidia wanafunzi wa Kituruki, alieleza.

“Je tunapaswa kuwa wajeuri kwa rais wa nyumbani wanakotoka familia zetu?” aliuliza.

“Kwa shutuma zozote zilizopo, sisi tuliamua kuonyesha ukarimu na upole kutokana na heshima kwa ofisi ya rais na kwa asili yetu ya Kituruki.”

Alisema “sio nia yetu kutoa ujumbe wowote wa kisiasa kwa picha hii”.

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mtanzania mwanaharakati Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Rebeca Gyumi Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *