Home / Habari za Kimataifa / Wapalestina wengine wawili wauawa Gaza

Wapalestina wengine wawili wauawa Gaza

Kijana akiwa ameshika ufunguo wa bandia wakati wa vurugu baina ya Waisrael na Wapalestina

.

Inaarifiwa kuwa Wapalestina wawili zaidi wamepigwa risasi na kufa katika ukanda wa Gaza wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa ukiendelea.

Akizungumzia na mkusanyiko wa mabalozi wa Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, ameisifu Israeli na kusema hakuna nchi itakayoweza kufanya zuio zaidi ya ilivyo.

Alisema kuwa kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas lilikuwa likihamasisha vurugu kwa miaka mingi.

Viongozi wa Palestina pamoja na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, walizungumza walipokuwa ziarani mjini London wameliita tukio la Jumatatu wiki hii kuwa ni mauaji ya kimbari.

Njia iliyotumiwa na Israeli ya kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji imelaumiwa duniani kote.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mtanzania mwanaharakati Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Rebeca Gyumi Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *