Home / Habari za Kimataifa / Ni nchi gani zinahamisha balozi zao kwenda Jerusalem

Ni nchi gani zinahamisha balozi zao kwenda Jerusalem

Mark Regev, balozi wa Israel nchini Uingereza.

Uamuzi wa Marekani kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem na kuutambua mji huo kuwa mji mku wa Israel umebadilisha sera ya Marekani ya miongo kadhaa.

Kwenye kipindi cha radio cha BBC balozi wa Israel nchini Uingereza Mark Regev alisema kufuatia uamuzi wa Marekani, kuna nchi za Kusini mwa Amerika na zingine za Uaya ambazo zinahamisha balozi zao kwenda Jerusalem.

“Ninaamini zingine zinafanya hivyo hivi karibuni,” alisema Bw Regev.

Huku kukiwa na shutuma za kimataifa kuhusu uamuzi wa Rais Trump, baadhi ya nchi, zimeunga mkono hatua hiyo na kusema kuwa zina mpango wa kuhamisha balozi zao.

Na nchi hizo ni zipi?

Kwenye mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa Disemba mwaka 2017, nchi tisa zikiwmo Marekani na Israel, zilipiga kura kupinga azimio la kuitaka Marekani kuondaa hatua ya kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

(Orodha kamili ni Marekani, Israel, Guatemala, Honduras, visiwa vya Marshal, Micronesia, Nauru, Palau na Togo.)

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mamfisa wa vyei vya juu wa White House Jared Kushner na Ivanka Trump walihudhuria

Nchi zikiwemo Uingereza, China, Ufaransa na Urusi na nchi zingine za Mashariki ya Kati ikiwemo Misri na Saudi Arabia zilipiga kura kuunga mkono azimio hilo.

Marekani ilifungua ubalozi wake mpya tarehe 14 mwezi Mei kwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 ya kuundwa taifa la Israel.

Wapalestina wa wanadai Jerusalem Masharikia kuwa mji wa mkuu wa baadaye na wananona hataua ya marekani kama ya kuunga mkono Israel kudhibiti mji huo wote.

Nchi zilizokuwa na balozi huko Jerusalem zilahamia Tel Aviv baada ya Israel kupitisha sheria mwaka 1980 ya kuutangaza mji wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu. Israel ilidhibiti eneo la mashariki la mji huo mwaka 1967 wakati wa vita vya mashariki ya kati katika hatua ambayo haikutambuliwa kimataifa.

Jengo la ubalozi wa Marekani mjini Tel Aviv

Tarehe 5 Machi rais wa Gatemala Jimmy Morales alitangaza kuwa angehamisha ubalozi wa nchi yake tarehe 16 mwezi Mei.

Aliandika kwenye Facebook: “Niliamua kurejesha ubalozi wa Guatemala kwenda Jurusalem siku mbili baada ya Marekani kuhamisha ubalozi wake.

“Huu ni uamuzi ulio huru na tunautambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Isarel.”

Wizara wa mashauri ya kigeni ya Israel ilisema Paraguay ina mpango wa kuhamisha ubalozi wake mwishoni mwa mwezi huu kwa mujibu wa Reuters.

Ripoti kutoka Times of Israel zilisema kuwa pamoja na Paraguay, nchi nyingine ya Amerika Kusini, Honduras inatarajiwa kuhamisha ubalozi wake.

Kulikuwa na maandamano kwenye ubalozi wa Israel huko Los Angeles

Uungwaji mkono wa Ulaya

Baada tangazo la Trump mwaka uliopita, Jamhuri ya Czech imesema kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa taifa la Israel kwenye mipaka yake ya mwaka 1967.

Hi inaamaanisha mipaka ya mwaka 1967 ambapo Israel ilitawala Jerusalem Magharibi huku Jordan ikidhibiti Jerusalem Mashariki.

Kumekuwa pia na ripoti za uungwaji mkono kutoka sehemu za serikali nchini Romania,.

Kwa mujibu wa gazeti la Israel la Haaretz nchi 32 kati ya 86 zilikubali mwaliko wa kusherehekea kufunguliwa kwa ubalozi wake mpya . Hizo ni pamoja na nchi za Ulaya, Hungary, Jamhuri ya Czech, Austria na Romania.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mtanzania mwanaharakati Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Rebeca Gyumi Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *