Home / Afya / Mambo 9 makuu kuhusu muda tunaoweza kuishi

Mambo 9 makuu kuhusu muda tunaoweza kuishi

Wanawake huishi miaka mingi kuliko wanaume kwenye nchi 195 na nchini Urusi wanawake huishi miaka mingi kuliko wanaume kwa miaka 11. Watu nchini Ethiopia wanaishi miaka 19 zaidi kuliko mwaka 1990 na watu walio kwenye nchi ambazo maisha yao ni marefu, wanaishi miaka 34 zaidi kuliko wale walio nchi ambazo watu huishi miaka michache.

Hayo ni baadhi ya matokeo ya hesabu za BBC kuhusu miaka ambayo watu huishi ambayo tumeyaonyesha kwenye chati zilizo hapo chini.

1. Tunaishi miaka mingi

Miaka ya watu kuishi duniani imeongezeka kwa zaidi ya miaka saba tangu mwaka 1990 ikiwa ni sawa na ongezeko la mwaka mmoja kwa kila miaka mitatu unusu.

Watu kote dunaini wanaishi miaka mingi na hii imetokana na kupungua kwa watu wanaokufa kutokana na ugonjwa wa moyo kwenye nchi za kipato cha juu na kupungua kwa vifo vya watoto kwenye nchi za kipato cha chini. Kuboreka kwa mfumo wa afya, usafi wa mazingira na matibabu bora kwa magonjwa pia vimechangia kuongezeka kwa miaka ambayo watu wanaishi.

Miaka ambayo unaweza kuishi ukiwa na afya nzuri pia iliongezeka kwa miaka 6.3. Hatahivyo kasi ukuwaji wa duniani imeanza kushuka tena.

2. Nchi za magharibi mwa Ulaya zinaongoza.

Kati ya nchi 20 za juu zenye miaka mingi ya kuishi 14 ziko barani Ulaya, lakini nchi za mashariki mwa Asia zinaongoza kwa ujumla: watu wanaozaliwa Japan na Singapore wanaweza kuishi miaka 84.

Uingereza pia nayo iko kwenye kundi la nchi 20 ambapo watu wanaishi miaka 81, huku Ireland Kaskazini ikichukua nafasi ya 32 na Wales 34 zote zikiwa na miaka 80. Scotland inachukua nafasi ya 42 kati ya nchi 198 ambapo watu huishi miaka 79.

3. Nchi za Afrika huchukua nafasi za chini

Nchi zote za mwisho 20 isipokuwa mbili tu ni za barani Afrika.

Watoto waliozaliwa mwaka 2016 nchini Lesotho na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wataishi miaka 50 tu, upungufu wa miaka 34 ya wale wanaozaliwa Japan.

Miongo kadhaa ya vita, ukame na ghasia zimefanya Afghanistan kuwa nchi pekee barani Asia kuwa miongoni mwa nchi ambazo watu huishi miaka michache ikiwa na miaka 58.

4. Wanawake wa jumla huishi miaka mingi kuliko wanaume.

Wanawake huishi miaka mingi zaidi kwenye nchi 195 kati ya nchi 198 kwa takriban miaka sita

Hata hivyo kwenye nchi nyingine mwanya uliopo ni miaka 11.

Kama chati inavyoonyesha, tofauti kubwa ya kijinsia iko mashariki mwa Ulaya na Urusi ambapo maisha mafupi ya wanaume yametajwa kuchangiwa na uraibu wa pombe na hali mbaya ya mazingira ya kazi.

Nchi tatu ambapo wanaume huishi zaidi kuliko wanawake ni Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, Kuwait na Mauritania.

5. Nchini Ethiopia, miaka ya kuishi iliongezeka kwa miaka 19

Tangu mwaka 1990 maisha yameimarika kwa asilimia 96 ya nchi.

Hapo awali watu waliozaliwa kwenye nchi 11 hawakutarajiwa kufika miaka 50 lakini tatizo hili lilitatuliwa na kila nchi mwaka 2016.

Sita kati ya zile zilishuhudia mabadiliko makubwa ni za kusini mwa jangwa la Sahara.

Ethiopia ambayo inajaribu kupata nafuu kutoka kwa ukame wa mwaka 1990, watu walikuwa na miaka 47 tu ya kuishi. Watoto waliozaliwa huko mwaka 2016 wanatarajiwa kuishi miaka 19 zaidi kutokana na kupungua kwa magonjwa ya kupumua na mengine kama kipindupindu.

6. Hata hivyo miaka ya kuishi ilishuka kwenye nchi nane

Licha ya kuwa nchi ambayo miaka ya kuishi iliongezeka, eneo la kusini mwa jangwa la sahara lina nchi nne kati ya nane ambapo miaka ya kuishi imeshuka sana tangu 1990.

Nchi ambazo miaka ya kuishi ilishuka zaidi ni Lesotho ambapo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kati ya watu wanne wanaishi na virusi vya ukimwi ikiwa ndiyo ya pili duniani iliyo na kiwango kama hicho.

Watoto waliozaliwa kwenye nchi jirani ya Afrika Kusini mwaka 2016 wanaweza kutararajiwa kuishi hadi miaka 62- miaka miwili chini ya wenzao waliozaliwa miaka 25 kabla au mwaka 1990.

Wakati wa kipindi hiki nchi hiyo imekabiliana na athari za kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi.

7. Tofauti za mipakani

Umri wa kuishi huenda unaweza kutajwa kwa eneo na eneo – baadhi ya nchi jirani zilikuwana tofuati ya hadi miaka 20 kati yao.

Mfano, ukivuka mpaka wa China kuingia Afghanistan, umri wa kuishi unapungua kwa miaka 18.

Na Mali – ambayo imekabiliwa na ugaidi na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka kadhaa – watu huishi kwa miaka 62 pekee , lakini watu wanaoishi katika nchi jirani ya Algeria wanaweza kutarajia kuishi hadi miaka 77.

8. Vita vina athari kubwa

Mnamo 2010, Syria iliorodheshwa ya 65 duniani kwa kiwango kikubwa cha kuishi, ikiwa katika thuluthi ya juu ya nchi zote. Hatahivyo kutokana na vita visivyomalizika vimeisbabaisha kushuka hadi katika nafasi ya 142 mnamo 2016.

Wakati huo huo, wakati mauaji ya kimbari yalipochacha Rwanda mnamo 1994, kadirio la umri wa mtu kuishi tangu azaliwe lilikuwa ni miaka 11.

9. Kama ilivyo kwa baa la njaa na majanga

Korea kaskazini ilikabiliwa na baa la njaa kati ya 1994 na 1998 iliyosababisha kupungua kwa umri wa mtu kuishi katika nchi hiyo hadi mapema mwaka 2000.

Zaidi ya watu 200,000 wanakadiriwa kufariki kutokana na tetemeko la ardhi Haiti mnamo 2010. Hatahivyo umri wa mtu kuishi katika nchi hiyo uliimarika mwaka uliofuata.

Je unataka kujua utaishi kwa muda gani zaidi duniani? Bonyeza hapa.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

WANAWAKE WATAKIWA KUNYONYESHA WATOTO MAZIWA YAO PEKEE

WANAWAKE wametakiwa kunyonyesha watoto maziwa ya mama pekee bila kuwapa maji, kinywaji au chakula kingine …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *