Home / Michezo / Urusi 2018: Neymar awekwa kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia licha ya jeraha

Urusi 2018: Neymar awekwa kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia licha ya jeraha

Brazil wamemtaka mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, ambaye bado anauguza jeraha, katika kikosi cha wachezaji 23 ambao wanatarajiwa kuchezea taifa hilo katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Neymar, 26, alifanyiwa upasuaji mwezi Machi na daktari wa timu ya taifa ya Brazil alisema hataweza kucheza kwa miezi mitatu.

Wachezaji wanne wanaochezea Manchester City Ederson, Danilo, Fernandinho na Gabriel Jesus ni miongoni mwa wachezaji wanaosakatia gozi Ligi ya Premia ambao wamo kwenye kikosi hicho.

Wengine ni nyota wa Liverpool Roberto Firmino na winga wa Chelsea Willian.

Beki wa kulia wa PSG Dani Alves atakosa michuano hiyo baada ya kupata jeraha la goti wiki iliyopita.

Brazil wamo Kundi E na Costa Rica, Serbia na Uswizi na watacheza mechi yao ya kwanza Jumapili 17 Juni.

Kikosi kamili cha Brazil:

Walinda lango: Alisson (Roma), Ederson (Manchester City), Cassio (Corinthians).

Mabeki: Danilo (Manchester City), Fagner (Corinthians), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis (Atletico Madrid), Thiago Silva, Marquinhos (both PSG), Miranda (Inter Milan), Pedro Geromel (Gremio).

Viungo wa kati: Casemiro (Real Madrid), Fernandinho (Manchester City), Paulinho (Barcelona), Fred (Shakhtar Donetsk), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Barcelona), Willian (Chelsea), Douglas Costa (Juventus).

Neymar ndiye mchezaji aliyenunuliwa ghali zaidi duniani

Washambuliaji: Neymar (PSG), Taison (Shakhtar Donetsk), Gabriel Jesus (Manchester City), Roberto Firmino (Liverpool).

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *