Home / Afya / Utafiti: Malazi ya Sokwewatu ni masafi kuliko ya binaadamu

Utafiti: Malazi ya Sokwewatu ni masafi kuliko ya binaadamu

Malazi ya Sokwemtu ni masafi zaidi kuliko ya binaadamu

Malazi ya Sokwe mtu ni masafi kuliko ya binaadam, wanasayansi wamebaini. Viumbe hawa hujenga malazi kwa kutumia matawi na majani ya miti ambapo hulala.

Malazi ya sokwe mtu ni mfano kwa mwanadamu kijana ambaye anaweza kuona vigumu kufuata

Mwanafunzi wa Marekani wa shahada ya Uzamivu Megan Thoemmes, aliyeongoza jopo kukusanya sampuli za uchafu kutoka kwenye Sokwe watu 41 katika bonde la Issa nchini Tanzania: ”Tunajua kuwa makazi ya binaadamu yana aina mbalimbali ya viumbe.

”Mfano, takriban asilimia 35 ya vijidudu kwenye vitanda vya binaadamu vinatoka kwenye miili yetu wenyewe, ikiwemo, kinyesi, kinywani na vijidudu vya kwenye ngozi

”Tulitaka kujua ni kwa namna gani hali hii inaweza kufananishwa na Sokwe hawa,ambao huandaa vitanda vyao kila siku.

Sokwe mzee zaidi kwenye hifadhi afariki Marekani

Kumbe sokwe sio wapenzi wa muziki

Ikilinganishwa na vitanda vya binaadamu, sehemu za kulala ya sokwe zilikuwa na aina mbalimbali za wadudu, matokeo ambayo hayakutarjiwa katika misitu ya kitropiki

Hata hivyo,uwezekano ni mdogo sana kwa sokwemtu kupata ”uchafu” kinyesi, kinywa au bakteria kwenye ngozi.

”Hatukuona vijidudu kwenye malazi ya Sokwe mtu, jambo lililoshangaza kidogo”, alieleza Bi Thoemmes kutoka Chuo cha North Carolina .

Walishangazwa na walichokigundua walipojaribu kusafisha malazi ya hao chimpanzee kuondosha viroboto na chawa waliokuwepo.

Watafiti wanasema vitanda vya Sokwe watu ni visafi zaidi kuliko vya binaadamu, ingawa viumbe hawa hutumia zaidi ya nusu siku kitandani.

Wanasayansi wamegundua kuwa malazi ya Sokwewatu nchini Tanzania yana kiasi kidogo cha kinyesi na bakteria kuliko magodoro ya binaadamu majumbani, kwa sababu viumbe hawa huhama malazi kila usiku.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Je maji ya madafu yana umuhimu gani katika mwili wa mwanadamu?

Madafu ni kinywaji maarufu sana pwani ya Kenya hasa mjini Mombasa. Kuanzia wenyeji mpaka watalii …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *