Home / Michezo / Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 17.05.2018

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 17.05.2018

Rafael Benitez

West Ham watazungumza na meneja wa Newcastle Rafael Benitez, huku naye meneja wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca kuwa miongoni kwa wale wanatafutwa. (Mirror)

Manchester United wanakaribia kumaliza makubaliano ya pauni milioni 43.7 na beki wa Juventus Mbrazili Alex Sandro, 27, huku mlinzi raia wa Italia Matteo Darmian, 28, akitarajia kuhamia Manchester United. (Le Stampa via Football Italia)

Manchester United nao wanamwinda beki wa Atletico Madrid raia wa Croatia Sime Vrsaljko, 26. (Mail)

Andre Silva

Wolves na Monaco wanammezea mate mshambulizi wa AC Milan raia wa Ureno Andre Silva, 22, ambaye alijiunga na Rossoneri kwa pauni milioni 33 msimu uliopita. (Sky Sports Italy – in Italian)

Arsenal wameanza kumtafuta mlinzi wa Borussia Dortmund raia wa Ugiriki Sokratis Papastathopoulos, 29, ambaye wanaamini kuwa watamsaini kwa pauni milioni 17.5 baada ya kuacha kumwinda raia wa Uturuki Caglar Soyuncu ambaye thamani yake ilitangazwa kuwa pauni milioni 35. (Mail)

Jonny Evans

Arsenal pia wana mpango wa kumsaini mlinzi raia wa Ireland Kaskazini Jonny Evans kwa pauni milioni 3 kufuatia kuzushwa kwa West Brom. (Mirror)

Mlinzi wa Stoke mwenye umri wa miaka 25 Kevin Wimmer, aliyesainiwa kutoka Tottenham kwa pauni milioni 18m msimu uliopia yuko kwenye mazungumzo kuhusu kuhamia klabu ya Ujerumani ya Hannover. (Mail)

Abel Hernandez

Mchezaji wa Hull City Abel Hernandez, 27, anaweza kuhamia Leeds wakati mkataba wake utamalizika baadaye msimu huu. (Yorkshire Evening Post)

Mlinzi wa Celtic Kieran Tierney, 20, anakiri kuwa anawindwa na Atletico Madrid lakini amedai atasalia Celtic hadi mwisho wa taaluma yake. (Herald)

Mchezaji wa Chelesea raia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema anasubiri kuona mazungumzo na Chelsea kanbla ya kusaini mkataba mpya. (Independent)

Bora kutoka Jumatano

Mauricio Pochettino

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino yuko tayari kuwakataa Chelsea kwa sababu anasema ana furaha kuwa na klabu yake. (Star)

Arsenal wamefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Nice Jean-Michael, 26, ambaye thamani yake ni pauni milioni 40. Lakini mahasimu wao wa London Chelsea wanaongoza mbio na kumsaini raia huyo wa Ivory Coast. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mikel Arteta, 36 anakaribia kuwa meneja mpya wa Arsenal akichukua nafasi ya Arsene Wenger baada ya mazungumzo kuendelea kati ya pande hizo mbili. (Independent)

Mikel Arteta

Nahodha wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira, 41, anasema amekasirishwa msh ahara ulionukuliwa na klabu hiyo baaada ya kuzungumziwa kuhusu nafasi ya umeneja iliyo wazi. (Sky Sports)

Manchester United wana uhakika wa kumsaini mlinzi Toby Alderweireld, 29, kutoka Tottenham. Red Devils wana nia ya kutumia pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji. (Evening Standard)

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *