Home / Habari za Kimataifa / Miguna Miguna ateuliwa naibu gavana Nairobi

Miguna Miguna ateuliwa naibu gavana Nairobi

Miguna Miguna

Gavana wa mji mkuu wa Kenya Nairobi Mike Mbuvi Sonko amemteua mwanasaisa wa upinzani anayekumbwa na utata Miguna Miguna kuwa naibu gavana.

Sonko alitoa tangazo hilo ambalo halikutarajiwa siku ya Jumatano jioni kwa njia ya barua kwa spika wa baraza la kaunti ya Nairobi, ikisema Miguna Miguna ametimiza matakwa yote yanayohitajika kikatiba.

Barua hiyo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua maoani mengi kutoka kwa wakenya, kutokana na kuwa uteuzi wake umekuja wakati ambao haukutarajiwa.

Miguna ambaye ana uraia wa Canada na Kenya, alitarajiwa kurudi nchini Kenya kutoka Canada baada ya kutimiliwa na serikali, lakini akaahirisha safari yake akisema kuwa idara ya uhamiaji huikumpa pasipoti halali jinsi ilivyoagizwa na mahakamma.

Bw Miguna Miguna (kwanza kushoto) wakati Bw Odinga alipokuwa anakula kiapo kuwa Rais wa Wananchi

Alitajarajiwa kuwasili Nairobi tarehe 16 mwezi huu licha ya kutimuliwa kutoka Kenya na serikali mara mbili katika kipindi cha miezi mitatu.

Alikuwa arudi nyumbani siku ambayo barua ya kuteuliwa kwake inaaminiwa kuandikwa.

Nafasi ya naibu gavana ilibaki wazi kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa naibu gavana Polycarp Igathe tayehe 12 Januari mwaka huu, kwa kile alichokitaja kuwa gavana kukosa kuwa na imani kwake kuhusu kusimamia masuala ya kaunti.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mtanzania mwanaharakati Rebeca Gyumi ashinda tuzo ya Umoja wa Mataifa

Rebeca Gyumi Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto kutoka nchini Tanzania Rebeca Gyumi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *