Home / Habari za Kimataifa / Washukiwa wa ufujaji wa pesa Kenya wafikishwa kortini Kenya

Washukiwa wa ufujaji wa pesa Kenya wafikishwa kortini Kenya

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji amesema upande wake utaiomba mahakama isiwaachie washukiwa kwa dhamana

Washukiwa 20 kati ya 50 waliokuwa wamekamatwa kutokana na sakata ya ufujaji wa Sh8 bilioni ($78m) kutoka kwa Shirika la Vijana wa Huduma kwa taifa (NYS) nchini Kenya wamefikishwa kortini.

Miongoni mwa walioshtakiwa ni Katibu Mkuu wa wizara ya masuala ya vijana na jinsia Lilian Mbugua Omollo na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw Richard ndubai.

Aidha, mameneja wa kampuni ambazo zinadaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo walifikishwa kortini Milimani, Nairobi.

Wanatarajiwa kujibu mashtaka mbalimbali yanayohusiana na kutoweka kwa $milioni 5 kati ya takriban dola milioni 80 zilizopotea katika shirika hilo la NYS.

Miongoni mwa mashtaka ambayo wamefunguliwa, ni makosa ya ulaghai, kutumia vibaya mamlaka na kula njama ya kutekeleza ufisadi.

Washukiwa zaidi wanatarajiwa kufikishwa kortini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji, alikuwa Jumatatu ametangaza kwamba idara yake itawafungulia mashtaka watumishi 40 wa umma na wafanyabiashara 14, pamoja na kampuni 10.

Washukiwa hao walikamatwa na wengine wakajisalimisha kwa polisi jana

Awali Haji alisema kuwa upande wake utaiomba mahakama isiwaachie kwa dhamana kwa wakati huu kuzuiwa jitihada zozote za uchunguzi wa kesi hiyo kuingilia kwa namna yoyote.

Wakenya wanaizungumziaje kesi

#MoneyLaunderingBanks na #NameTheRealNYSThieves ni mada mbili kuu zinazozungumziwa pakubwa katika mitandao ya kijamii Kenya.

Katika Twitter mada hizo zimegubika mazungumzo kuhusu mabenki yaliotumika nchini kufanikisha malipo kwa makampuni kadhaa yaliohusishwa katika kashfa hiyo ya takriban dola milioni 80.

Jamaa huyu katika ujumbe wake hapa anasema hii sio sura mtu anayoweka wakati anajua ataadhibiwa kwa uhalifu.

Vyombo vya habari nchini vinaripoti kwamba katibu mkuu katika idara ya umma nchini Lilian Omollo ambaye ni mojawapo ya washtakiwa, na Richard Ndubai mkurugenzi mkuu wa NYS wamekana mashtaka ya kuwa na njama ya kulilaghai shirika la NYS fedha kiasi cha Shilingi milioni 28.7 ambazo zilitajwa kuwa ni malipo kwa kampuni ya Ameri Trade Limited.

Utakatishaji wa fedha

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya amesema huenda baadhi ya benki zilikiuka sheria za kukabiliana na utakatishaji wa fedha katika kutolewa kwa fedha ambazo zinadaiwa kuibiwa kutoka kwa NYS.

Bw Patrick Njoroge amesema benki hiyo inashirikiana na polisi katika uchunguzi wa wizi huo wa karibu $100m.

Shirika la NYS limekuwa likishirikishwa sana katika mpongo wa serikali ya Kenya wa kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.

 

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

DSTV, AZAM na ZUKU zatakiwa kuonyesha bure vipindi vya stesheni za Tanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe Waziri wa Habari, Utamaduni, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *