Home / Michezo / Liverpool yamsajili Fabinho kwa Paundi Milioni 40

Liverpool yamsajili Fabinho kwa Paundi Milioni 40

Fabinho anatarajia kuchukua nafasi ya Emre Can ambaye anatimkia Juventus

Liverpool imekubali kumsajili kiungo wa Monaco Fábio Henrique Tavares maarufu kama Fabinho kwa ada ya Paundi Milioni 40 ambayo inaweza kuongezeka kutokana na kiwango cha mchezaji.

Fabinho mchezaji wa kimataifa wa Brazil mwenye miaka 24 atajiunga na Liverpool Julai 1.

Kiasi cha ziada cha ada ya uhamisho wake ambacho ni Paundi Milioni 5 kinaweza kuongezeka kutokana na mafanikio atayoipa Liverpool.

Kuwasili kwake ni kwa ajili pia ya kuziba pengo la Emre Can ambaye anatarajiwa kutimkia kwa mabingwa wa Seria A Juventus muda wowote.

Fabinho alijiunga na Monaco akitokea Rio Ave ya Ureno mwaka 2013

”Hiki ni kitu ambacho sikuzote nimekuwa nikikitamani- hii ni timu kubwa, ”alisema Fabinho. ”Nimefurahishwa sana.”

Fabinho: Mwaliko wa Mourinho unaweza ”kunishawishi”

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ”Huyu ni mchezaji ambaye ana faida sana uwanjani, anaweza kucheza nafasi nyingi, namba sita, nane ama namba mbili’. Hili ni jambo zuri sana.”

Fabinho ambaye mkataba wake unatarajiwa kuanza Julai 1 amesema Liverpool ni klabu yenye miundombinu mizuri na ya kuvutia.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *