Home / Michezo / Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 29.05.2018: Mahrez anatafutwa na Man City, Mourinho wasiwasi juu ya Gareth Bale

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 29.05.2018: Mahrez anatafutwa na Man City, Mourinho wasiwasi juu ya Gareth Bale

Manchester City wanamtafuta mchezaji wa Algeria Riyad Mahrez msimu ujao

Manchester City wanakaribia kukamilisha ununuzi wa pauni milioni 75 kwa ajili ya winga raia wa Algeria Riyad Mahrez, mwenye umri wa miaka 27, kutoka Leicester City. (Mail)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana hofu juu ya ushindani wa malipo ya kifedha usajili wa mchezaji wa Wales Gareth Bale kutokana na bei yake, huku Real Madrid ikitarajiwa kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa bei ya pauni milioni 200 (Express)

Liverpool wako tayari kujiandaa kusaini mkataba na nahodha wa timu ya Lyon Nabil Fekir huku mzungumzo kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba wa pauni milioni 60 na mchezaji huyo wa safu ya kati mwenye umri wa miaka 24 yakitarajiwa kuanza wiki hii. (Goal)

Jose Mourinho ana hofu juu ya ushindani wa malipo ya kifedha ya usajili Gareth Bale

Mkurugenzi wa soka wa Roma Monchi anasema kuwa hakuna lengo lolote la kumuuza mlinda lango wao Alisson.

Mlinda lango huyo nambari moja mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akihusishwa na Liverpool, na taarifa hizo ziliongezeka baada ya kushindwa katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (Mirror)

Manchester United wanamfuatilia kwa karibu mchezaji wa safu ya kati ya Aston Villa Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 22, huku wakiangalia namna ya kujijenga siku zijazo. (Sun)

Mlinzi wa Atletico Madrid Sime Vrsaljko anasema anafurahia kuchezea klabu yake Uhispania, licha ya kwamba Manchester United wanamsaka

Manchester City wamekataliwa kumnunua mchezaji wa kiungo cha kati wa Napoli Jorginho kwa pauni milioni. Klabu hiyo ya Ligi kuu ya Italia (Serie A ) wanataka walipwe pauni milioni 52 kwa mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 26, na wanakabiliwa na ushindani kutoka upande wa Chelsea. (Mirror)

Juventus inaweza kumruhusu mshambuliaji Gonzalo Higuain kuondoka kwneye klabu hiyo, ikiwa watapata mkataba unaofaa msimu huu, huku Chelsea wakioongoza katika kutimiza vigezo vya kumchukua raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 30. (Calciomercato)

West Ham wako makini kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Fiorentina Milan Badelj. Badelj mwenye umri wa miaka 29 hana mkataba msimu huu, lakini klabu hiyo ya Italia inaamini atasaini mkataba mpya. (Tutto Mercato Web)

Newcastle ina fursa ya kusaini mkataba na mlizi wa zamani wa Liverpool Martin Skrte

Mlinzi wa Atletico Madrid Sime Vrsaljko anasema anafurahia kuwa klabu hiyo ya Ligi ya Uhispania, licha ya taarifa kwamba Manchester United wanataka kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, na mchezaji wa kimataifa wa Croatia. (Sportske Novosti – in Croatian)

Newcastle wamepewa fursa ya kusaini mkataba na mlinzi wa zamani wa Liverpool Martin Skrtel, mwenye umri wa miaka 33, kutoka Fenerbahce msimu huu. (Fotomac)

Samuel Umtiti anayesakwa na Manchester United amefichua taarifa kuhusu utashi wake wa kubakia Barcelona

Manchester City wako tayari kukamilisha mkataba na Paris St-Germain kwa ajili ya mshambuliaji wa timu ya Monaco mwenye umri wa miaka 19 Kylian Mbappe.

Mfaransa huyo alikuwa katika timu ya PSG kwa mkopo msimu uliopita lakini mabingwa hao wa Ufaransa huenda wakalazimika kuvunja mpango wao wa kumsaini (Manchester Evening News)

Wakili wa Misri amewasilisha kesi ya pauni bilioni moja dhidi ya Sergio Ramos kuhusiana na kujeruhiwa kwa Mo Salah katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Samuel Umtiti anayesakwa na Manchester United amefichua taarifa kuhusu utashi wake wa kubakia Barcelona. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24 anayecheza safu ya kati – nyuma anasema kuwa hataondoka klabu hiyo ya Uhispania labda afukuzwe. (Sun)

Wakili wa Misri amewasilisha mashtaka ya pauni bilioni moja dhidi ya Sergio Ramos kuhusiana na namna Mohamed Salah alivyoumia katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Evening Standard)

Meneja wa timu ya Uholanzi Ronald Koeman na kikosi chake wamekuwa wakifurahia masomo ya mchezo wa vishale kutoka kwa raia wa Uholanzi Michael van Gerwen. (Twitter)

Mlinda lango wa Manchester Joe Hart, mwenye umri wa miaka 31, amebadilisha mawakala wake baada ya kutupwa nje ya kikosi kitakachoiwakilisha England katika michuano ya Kombe la Dunia. (Mail)

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *