Home / Habari Za Kitaifa / TSN yaombwa majukwaa ya kisekta Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko masaa 11 yaliyopita

TSN yaombwa majukwaa ya kisekta Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko masaa 11 yaliyopita

WADAU mbalimbali mkoani Arusha wameitaka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayoandaa majukwaa ya fursa za kibiashara kuandaa majukwaa yatakayojumuisha wadau wa sekta za ardhi na kilimo.

Kampuni ya TSN wanaochapisha gazeti hili na ya HabariLeo, Dailynews na Spotileo ndiyo waandaaji wa majukwaa hayo ya kibiashara, na wiki iliyopita walifanya jukwaa la sita mkoani Arusha, baada ya kufanyika mengine matano katika mikoa ya Simiyu, Tanga, Shinyanga, Mwanza na visiwa vya Zanzibar.

Wameeleza kuwa majukwaa hayo yanayotoa fursa za wazi kwa wananchi kutoa kero zao na kupatiwa majibu papo hapo yameonesha mafanikio makubwa katika sekta nyingi hivyo kubaki changamoto katika masuala ya ardhi na kilimo.

Akizungumzia majukwaa hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya KBS Logistics ,Walter Maeda alisema ni vema kushirikisha wahusika katika kilimo ili kupata ufumbuzi wa usafirishaji wa mazao nje ya nchi pamoja na umiliki wa ardhi na jinsi ya kupata hati.

Jambo lililoungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Projam, Prosper Mwendi aliyekiri kupata kitu kikubwa kupitia jukwaa hilo kupitia taasisi za fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini akaomba kuandaliwa jukwaa lingine linalohusu masuala ya kilimo, madini pamoja na ardhi na kuletwa wahusika kwa lengo la kupatia ufumbuzi changamoto zilizopo.

“Mkoa wetu umekuwa na shughuli nyingi za madini, kilimo na hata ufugaji, wakati TSN wanajiandaa kwa ajili ya majukwaa ya kisekta ni vema kuleta wahusika wa masuala haya ili tuweze kupata majibu ya changamoto zilizopo kama walivyofanya TRA kwenye jukwaa hili,” alisema.

Katika Jukwaa hilo la fursa za biashara Arusha wananchi wengi walieleza kero zao kuhusu masuala ya upatikanaji wa mitaji katika mabenki, changamoto za ulipaji kodi pamoja na masuala ya uwekezaji na kupata majibu kutoka kwa wahusika.

Mkurugenzi wa Masoko wa benki ya TIB Corporate, Theresia Soka alitaka wananchi kutembelea benki yao mkoani hapo ili kusaidia katika uwekezaji wa masuala mbalimbali pamoja na kupata mikopo yenye riba nafuu.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *