Home / Michezo / Msanii wa Bongo Fleva Tanzania Sam wa Ukweli ameaga dunia

Msanii wa Bongo Fleva Tanzania Sam wa Ukweli ameaga dunia

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Sam wa ukweli

Msanii wa Bongo Fleva, Salum Mohamed aliyetamba kwa jina la Jukwaani kama Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 7, 2018.

Sam alitamba sana na kazi zake kama vile Sina Raha alioutoa katika ya mwaka 2009 na 2010, Usiniache, Lonely na Hata kwetu wapo.

Hapo kati kati alipotea mpaka mwishoni mwa mwaka 2017 alipoibuka na kibao kingine kwa jina Kisiki na baadaye mwanzoni mwaka huu wa 2018 akauachia Wimbo Ni Wewe.

Ingawa ni mtu wa Singida Sam wa Ukweli amekulia Kiwangwa jirani na mji wa Dar es Salaam ambako amelelewa na Bibi yake mzaa mama.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Meneja wa msanii huyo, Abdulmalik Mohamed , mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na mipango ya mazishi inaendelea katika eneo la Tandale lakini Maziko yatafanyika Alhamis hii Kiwangwa mkoani Pwani.

Aidha meneja huyo amesema chanzo cha kifo cha msanii huyo ni Malaria na UTI (Urinary Tract Infection) ya muda mrefu.

Sam alikuwa akiandaa nyimbo zake mpya kabla ya kuanza kusumbuliwa na Tumbo akiwa Studio.

Ameacha mke na mtoto mmoja wa kike.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Man United iko mbioni kumtangaza Mkurugenzi wa michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *