Home / Uncategorized / Ukarabati wa Jumba la Treni

Ukarabati wa Jumba la Treni

Jumba La Treni, Zanzibar

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema, ukarabati wa jengo refu maarufu la treni lililopo Darajani eneo la Mji Mkongwe, unaendelea vizuri na umefikia asilimia 70.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Khalid Salum Mohamed ameyasema hayo wakati anatoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya jengo hilo.

Dk Mohamed alisema ukarabati wa jengo hilo unafanywa na kampuni ya Kichina ya CRJ iliyosajiliwa nchini baada ya kushinda zabuni ya ujenzi wa mradi huo.

”Ujenzi wa mradi wa jengo la treni unaendelea vizuri ukiwa umekidhi vigezo vyote vinavyotakiwa kwa mujibu wa maelekezo ya Mamlaka ya hifadhi ya Mji Mkongwe pamoja na Unesco,”amesema.

Amesema jengo hilo litakuwa na uwezo wa lifti mbili zitakazofanya kazi, ambapo kwa mujibu wa utafiti wa Mji Mkongwe litakuwa na uwezo wa kudumu zaidi ya miaka 100.

Aidha, alisema mradi huo umegharimu Sh bilioni 11.2 ambapo serikali inatarajiwa kukabidhiwa jengo hilo mwezi ujao baada ya kukamilika taratibu zote za ujenzi na mikataba ambapo mjenzi tayari amelipwa asilimia 59 ya fedha anazodai kwa mujibu wa mkataba.

Alisema mara mradi huo utakapomalizika, wahusika wote waliokuwepo awali ambao ni wapangaji waliokuwa wakifanya biashara wataitwa na kupewa taarifa rasmi.

Alifahamisha wafanyabiashara waliokuwepo awali ndiyo watakaopewa kipaumbele cha kwanza kama watakubaliana na vigezo na makubaliano na wahusika ambao ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(ZSSF).

”Hakuna mkubwa aliyechukua milango ya maduka hadi sasa, wahusika waliokuwepo awali ndiyo watakaopewa kipaumbele cha kwanza kama watakubaliana masharti na wamiliki wa jengo hilo,”alisema.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Gambia akamatwa

Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh Maafisa wa polisi nchini Gambia wamemkamata aliyekuwa kiongozi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *