Home / Habari Za Kitaifa / ANDENGENYE APANGUA MAKAMANDA ZIMAMOTO

ANDENGENYE APANGUA MAKAMANDA ZIMAMOTO

MKUU wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini (CGF) Thobias Andengenye amefanya mabadiliko ya ya Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vitengo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hapa nchini. Mabadiliko hayo yamelenga kuongeza ufanisi katika kupambana na majanga ya moto na majanga mengine yanayoendelea kutokea maeneo mbalimbali hapa nchini.

Katika kuendana na mabadiliko hayo CGF Andengenye amewataka pia makamnda wote wa jeshi la zimamoto na uokoaji mikoa kuhakikisha wanasimamia vyema dhima ya jeshi hilo la uokoaji maisha na mali ili kupunguza majanga ya moto yanayoathiri Watanzania na kurudisha juhudi za maendeleo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Makao Makuu, Inspekta Joseph Mwasabeja ilisema kuwa katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi(ACF) Fikiri Salla anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto(RFO) Mkoa wa Dodoma, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi(ACF) Abdallah Maundu aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto(RFO) mkoa wa Katavi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi(ACF) Regina Kaombwe ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto(RFO) mkoa wa Dodoma.

Iliendelea kusema kuwa Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Juma Kwiyamba aliyekuwa Makao Makuu Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto (RFO) mkoa wa Mwanza ambaye anajaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Mwanza kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyekuwa Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi (ACF) Mohamed Kondo anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Peter Mabusi ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Zimamoto Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Kamanda wa Zimamoto(RFO) mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi (ACF) Saidi Geugeu anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Lindi, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi(ASF) Christina Sunga ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto(RFO) mkoa wa Lindi.

Iliendelea kusema kuwa Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Yange aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Zimamoto Kiwanja cha Ndege (JNIA)anakuwa Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini wakati Kamishna Msaidizi wa Zimamoto (ACF) Maria Kullaya aliyekuwa Makao Makuu Dar es Salaan anakwenda kuwa Mkuu wa Kituo cha Zimamoto Kiwanja cha ndege(JNIA).

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Kamanda wa Zimamoto(RFO), mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi (ACF) Gilbert Mvungi anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Morogoro, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Athuman Basuka ambaye alikuwa Mkuu wa Kituo cha Zimamoto Mkoa wa Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kamanda wa Zimamoto(RFO), Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi (ACF) Baraza Mvano anakwenda kuwa Mkuu wa Kituo cha Songwe Airport, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi(ASF), Hamisi Rutengo aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto (RFO) mkoa wa Singida na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi(ASF) Ivo Ombella kutoka makao makuu.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Zimamoto (SSF) Chrispin Rabiuzima aliyekuwa Makao Makuu Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto(RFO) Mkoa wa Simiyu ambapo anachukua nafasi ya Kamanda wa Zimamoto Mkaguzi (INSP) Gervas Fungamali aliyehamishiwa Makao Makuu kitendo cha Usafirishaji.

Wengine waliobadilishwa ni Kamanda wa Zimamoto (RFO) mkoa wa Kagera, Mrakibu Mwandamizi wa Zimamoto (SSF) George Mrutu amehamishiwa Makao Makuu ya Zimamoto Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Idd Telemkeni kutoka makao makuu. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Mrakibu Msaidizi (ASF) Puyo Nzalayaimisi aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto Kigamboni anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto (RFO) mkoa wa Temeke akichukua nafasi ya Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Loshpay Laizer ambaye amehamishiwa Makao Makuu.

Iliendelea kusema kuwa aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Ilala(RFO), Mrakibu Msaidizi (ASF) Ully Mbuluko amehamishiwa makao makuu kitengo cha operesheni, kamanda wa zimamoto mkoa wa Geita (RFO), Mrakibu Msaidizi Elisa Mugisha akienda kuwa Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Ilala na nafasi yake ikichukuliwa na Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Zabrone Muhumha kutoka makao makuu.

Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto (ASF) Isabela Mbwago aliyekuwa Kanda Maalumu Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Zimamoto (RFO) mkoa wa Rukwa akijaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya Kamanda wa Zimamoto Rukwa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Katika mabadiliko hayo pia aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Zimamoto mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Msaidizi (ASF) Ambwene Mwakibete amekuwa Kamanda wa Zimamoto (RFO) mkoa wa Kinondoni.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *