Home / Habari Za Kitaifa / RAIS ATUNUKU KAMISHENI LUTENI USU 118

RAIS ATUNUKU KAMISHENI LUTENI USU 118

RAIS Dk John Magufuli amewatunuku kamisheni za cheo cha Luteni usu maofisa wa jeshi 118 kati 123 waliomaliza mafunzo ya kijeshi katika Vyuo vya Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha na nchini India.

Dk Magufuli ametunuku kamisheni hizo jana katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo kati ya wahitimu 123, wahitimu 118 ni watanzania na wahitimu watano wametoka katika nchi za Uganda, Rwanda na eSwatini (Swaziland). Akizungumza baada ya Rais Dk Magufuli kukabidhi kamisheni hizo Mkuu wa Chuo Cha Mafunzo ya kijeshi Monduli, Luteni Jenerali Paul Massao alisema wahitimu hao wa kozi ya 63 ya mwaka 2017 walianza kozi Julai 3, mwaka jana na kumaliza jana ambapo idadi ya waliohitimu imetoka miongoni kwa wanafunzi 183 waliojiunga na mafunzo hayo ambapo kati yao wanaume walikuwa 176 na wanawake saba.

Alisema kati ya wanafunzi 183 waliochaguliwa kwenda mafunzo, wanafunzi 87 walishindwa mafunzo kwa sababu mbalimbali zikiwemo magonjwa, utovu wa nidhamu, kushindwa kuhudhuria mafunzo kwa siku 14 na wengine waliandika barua za kutaka kuacha mafunzo kwa hiari yao. “Waliotunukiwa kamisheni leo wapo watanzania 118, kati ya hao wanaume 115 wanawake watatu, wamo pia watano kutoka mashirika ya nje ambapo watatu wametoka nchi ya eSwatini(Swaziland) watatu,Uganda mmoja na Rwanda mmoja,”alisema Luteni Jenerali Massao.

Alisema wahitimu waliotunukiwa kamisheni jana mbali ya kupitia kozi hiyo pia wana sifa mbalimbali za kielimu ambapo miongoni mwao wapo wenye shahada ya uzamili (Masters), shahada ya kwanza (Bachelor Degree), Astashahada ya juu (Advanced Diploma), Stashahada (diploma) pamoja na wahitimu wenye elimu ya kidato cha sita.

Kabla ya kukabidhi Kamisheni hizo Rais Magufuli alikabidhi zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika nyanja mbalimbali wakiwa katika kozi hiyo. Miongoni mwa waliokabidhiwa zawadi hizo ni pamoja na Daniel Meshack ambaye alitajwa kama mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kwenye mafunzo hayo wakati Henry Kakuba alikabidhiwa zawadi ya mwanafunzi bora aliyefanya vizuri darasani. Zawadi ya mwanafunzi bora katika medani ilikabidhiwa kwa Ramadhani Kakombe wakati aliyepata zawadi ya mwanamke aliyefanya vizuri zaidi ni Beatrice Kipinge huku mwanafunzi aliyefanya vizuri kutoka nchi za kigeni zilizoshiriki mafunzo hayo ni Amstrong Bitegeya kutoka nchini Uganda.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *