Home / Habari za Kimataifa / Mtoto wa miaka miwili afariki baada ya kujipiga risasi Texas, Marekani

Mtoto wa miaka miwili afariki baada ya kujipiga risasi Texas, Marekani

Christopher Williams Jr na babake
Mtoto wa umri wa miaka miwili nchini Marekani amefariki baada ya kujipiga risasi kichwani kwa bunduki ambayo imekuwa ikihifadhiwa na wazazi wake nyumbani kwao.

Polisi wa Houston, Texas wanasema wazazi wa mtoto huyo – Christopher Williams Jr – walikuwa nyumbani wakati wa kutokea kwa kisa hicho.

Polisi wanasema bunduki hiyo ambayo hutumia risasi za ukubwa wa 9mm ilipatikana eneo la tukio na kwamba ilikuwa inamilikiwa na babake.

Kufikia sasa, bado haijabainika iwapo wazazi wake watashtakiwa.

Mganga aliyedai kuwa na nguvu za kuzuia risasi afariki kwa kupigwa risasi
Mtoto wa miaka 9 amuua nduguye kwa risasi Marekani
Watoto kadha wamekuwa wakijipiga risasi na kujiua kimakosa nchini Marekani miaka ya karibuni.

Polisi wa Houston wamesema wanajaribu kubaini ni vipi mtoto huyo aliyepewa jina la utani “Junior” aliweza kuifikia bunduki hiyo.

Mkuu wa kitengo cha waathiriwa maalum katika idara ya polisi ya Houston David Angelo ametoa wito kwa wazazi walio na bunduki kuchukua tahadhari zaidi.

“Ni lazima uweke salama silaha, iwe ni kwa kuhakikisha kifaa cha kufyatulia risasi kimewekwa salama au kuiweka salama silaha kwa njia nyingine kuhakikisha matukio kama haya hayatokei tena siku za usoni,” alisema.

Alieleza kisa hicho kuwa cha kusikitisha sana.

Binamu yake marehemu Suzzane Alvarado ameambia ABC 13 kwamba marehemu “hakustahili yaliyomkuta. Alikuwa mtoto mdogo na mwenye matumaini makubwa maishani.”

Kwa mujibu wa gazeti la Houston Chronicle, babake marehemu Christopher Charles Williams, alipatikana na hatia ya kuwa na bastola kinyume cha sheria mwaka 2009.

Christopher Williams Jr, alifariki Jumapili Houston.
Bi Alvarado alimweleza kama baba mwenye kuwajibika sana kwa mwanawe.

“Saa 24 kwa siku, alikuwa na mwanawe. Alikuwa akifanya zaidi ya kina baba wengine.”

Jumatatu, polisi Houston walimshtaki baba mwingine kutokana na kujipiga risasi kimakosa kwa mwanawe wa kiume mwezi Mei.

Ali Parvez Masoom, 32, anadaiwa kuiacha bunduki yake aina ya .308 mezani ambapo mwanawe aliweza kuifikia na kujipiga risasi usoni.

Mtoto azaliwa na risasi mwilini nchini Marekani
Mwanamke anayejiita ‘mungu’ aliyewapiga watu risasi India
Bw Massom aliachuliwa huru baada ya kulipa dhamana ya $1,000 (£750) na kwa sasa anakabiliwa na kosa la kutowajibika na kumuwezesha mtoto kuifikia silaha.

Jumamosi, mtoto mwingine wa miaka miwili alifariki Fresno, California katika kisa karibu sawa na hicho.

Wazazi wa mtoto huyo walikuwa nyumbani alipoifikia bastola hiyo na kujipiga risasi kichwani.

Unaweza kusoma pia:
Kwa nini raia hawawezi kupokonywa bunduki Marekani
Trump ‘aunga mkono’ uboreshaji wa ukaguzi wa silaha
IS wanatumia ndege zisizo na rubani Iraq

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *