Home / Habari za Kimataifa / Marekani imeshindwa kuwarejesha watoto wa wahamiaji kwa wazazi wao

Marekani imeshindwa kuwarejesha watoto wa wahamiaji kwa wazazi wao

Mmoja wa watoto wa wahamiaji nchini Marekani akisubiria kuunganishwa na wazazi wake
Serikali ya Marekani imesema itashindwa kuwaunganisha watoto wa wahamiaji na wazazi ndani ya muda uliopangwa na mahakama. Mamia ya watoto hao walitenganishwa na mara baada ya kukamatwa katika mpaka wa Mexico na Marekani kama wahamiaji walioingia bila kufuata sheria za uhamiaji.

Kwa sasa watoto hao wenye umri wa miaka wa chini ya miaka mitano wanahifadhiwa katika mazingira yenye utata kwa mjibu wa mashirika ya haki za watoto

Wahamiaji 112 wakamatwa Mexico wakielekea Marekani
Waziri wa Marekani,Mexico wakutana
Pamoja na kuelezea wasiwasi wake wa kutimiza amri ya mahakama serikali ya Marekani imesema kuwa watoto 34 leo wataunganishwa na wazazi wao.Lakini wamesema ni ngumu kwa watoto wengine kutokana na taratibu za kiusafiri.

Serikali ya rais Trump inasema kuwa watoto wengine haitakuwa rahisi kuwaunganisha na wazazi wao kwa sababu baadhi ya wazazi wao wanakabiliwa na mashitaka na wapo kwenye vizuizi.

Lee Gelernt ni mwanasheria ambaye kwa kushirikiana na mashirika mengine walifungua kesi dhidi ya serikali kuhakikisha watoto hawa wanarejeshwa kwa wazazi wao,anasema kuwa anasikitishwa kuona serikali haijatekeleza amri ya mahakama hadi sasa.

“Tumekatishwa tamaa kiasi kikubwa,kuona kwamba serikali inaonekana kama haitaweza kuwaunganisha watoto hawa na wazazi wao leo.Lakini tunaamini kwamba kwa kuwa Jaji amehusishwa katika mchakato huu tangu siku ya ijumaa,ufuatiliaji utaendelea.Na tunaamini kwamba kuanzia sasa muda wa mwisho uliowekwa utaheshimiwa. “Lee Gelernt

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya safari yake mjini Brussels Ubelgiji kuhudhuria mkutano wa NATO,rais Trump amesisitiza ufumbuzi dhidi ya muda uliowekwa ni rahisi.

“Ndiyo nina ufumbuzi,waambieni watu,wasiingie nchini kwetu kinyume cha sheria,usije nchini kwetu kinyume cha sheria,njoo kama watu wengine waoingia kisheria.”Trump.

Takriban watoto 3,000 walitenganishwa na wazazi wao,ambapo hapo jana July 10 serikali ya Marekani ilipaswa kuwa imewarejesha watoto hao kwa wazazi wao.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Mohamed Bin Salman

CIA ‘yamlaumu mwanamfalme wa Saudia ‘

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *