Home / Michezo / Tetesi za soka Ulaya Jumatano 11.07.2018

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 11.07.2018

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo atakuwa akipokea takriban £73,000 kwa siku huku mkataba wake wa miaka minne ukiwa na thamani ya £26m kwa mwaka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na mabingwa hao wa Itali kutoka Real madrid kwa dau la £99.2m. (Mirror)

Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Fabio Capello anasema kuwa hatua ya Ronald kujiunga na Juventus ni ya kijanja. Raia huyo wa Itali sasa anatarajia kwamba mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain, 30, ataelekea Chelsea. (Football Italia)

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 27, anapigiwa upatu na wachanganuzi wa soka kuchukua mahala pake Ronaldo katika klabu ya Real Madrid – na raia huyo wa Ubelgiji ataondoka Stamford Bridge iwapo Chelsea haitaonyesha ari ya kutaka kununua wachezaji wapya(Football London)

Riyad Mahrez ajiunga na Manchester City
Hatua hiyo ya Ronaldo itaiwezesha Juventus kuuza wachezaji ili kuafikia sheria za Fifa – na kiungo wa kati wa Itali Stefano Sturaro, 25, amevutia klabu za Newcastle na Wolves. (Birmingham Mail)

Liverpool iko tayari kumununua mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 24, kwa dau la £80m . (TyC Sports, via Metro)

Liverpool imeanzisha mazungumzo na Stoke kuhusu mkataba wa kumnunua kiungo wa kati wa Switzerland mwenye umri wa miaka 26 Xherdan Shaqiri, ambaye anaaminika kuwa na thamani ya £13m katika kandarasi yake . (Telegraph)

Tottenham na Roma wako tayari kumnunua mchezaji wa Bordeaux na Brazil Malcom, 21. (France Football – in French)

Everton iko tayari kutoa dau la £21m ili kumnunua beki wa kati wa Barcelona na Colombia Yerry Mina, 23. (Goal)

Mfahamu Samuel Umtiti aliyewafikisha Ufaransa fainali Kombe la Dunia
Liverpool inatafakari kumnunua mchezaji wa Poland Grzegorz Krychowiak. Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 28 alihudumu msimu uliopita akiwa katika klabu ya West Brom kwa mkopo kutoka Paris St-Germain. (Sun)

Mkufunzi wa Napoli Carlo Ancelotti amemshirikisha beki wa Brazil na Chelsea David Luiz, 31, katika orodha ya wachezaji anaowalenga. (Mirror)

Southampton itakamilisha makubaliano ya kibinafsi na beki wa Borussia Monchengladbach Jannik Vestergaard baada ya raia huyo wa Denmark , 25, kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu kwa uhamisho wa dau la £18m . (Sky Sports)

Cristiano Ronaldo atua Juventus

Leicester imejiandaa kumpatia beki wa Uingereza Harry Maguire, 25, mkataba mpya ili kumfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa bora zaidi (Leicester Mercury)

Fulham huenda ikaipiku Chelsea na Arsenal katika kumsajili kiungo wa kati wa Ivory Coast Jean Michael Seri, 26. (Sun)

Mshambuliaji wa Sunderland na Tunisian Wahbi Khazri, 27, ameamua kuhamia katika klabu ya ligi ya Ufransa ya Saint-Etienne. (Le Progres, via Sports Witness)

Newcastle inakaribia kumsani kwa mkopo wa muda mrefu kiungo wa kati wa Chelsea Kenedy baada ya raia huyo wa Brazil, 22, kukamilisha ukaguzi wa matibabu. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Newcastle Rafa Benitez anasema kuwa hataki kumuuza nahodha wa klabu hiyo Jamaal Lascelles baada ya mchezaji huyo wa Uingereza ,24, kuhusishwa na West Ham. (Newcastle Chronicle)

Lille ina hamu ya kumnunua kipa wa Everton na Uholanzi Maarten Stekelenburg, 35. (France Football, via Talksport)

Mchezaji anayelengwa na Arsenal Gelson Martins, 23, anakaribia kujiunga na Atletico Madrid. Mchezaji huyo wa Ureno anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake wiki hii. (Record)

Arsenal huenda ikamkosa kipa wake David Ospina, 29, huku Boca Juniors wakitarajiwa kukamilisha uhamisho kwa makubaliano ya dau la £6m. (Mirror)

Lyon inamnyatia winga wa West Brom na Ubelgiji Nacer Chadli, 28. (France Football, via Talksport)

Beki wa Uhispania Joel Lopez, 15, amethibitisha anaondoka Barcelona huku kukiwa na uvumi kwamba anahamia Arsenal. (Football London)

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *