Home / Michezo / Riyad Mahrez ajiunga na Manchester City kwa Paundi milioni 60

Riyad Mahrez ajiunga na Manchester City kwa Paundi milioni 60

Mahrez ameelezea kiwango cha Manchester City msimu uliopita kuwa cha maajabu
Manchester City imevunja rekodi yake kwa kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez kwa Paundi milioni 60.

Mahrez mwenye miaka 27 amesaini mkataba wa miaka 5 na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na City tokea ichukue ubingwa msimu uliopita.

City ilijiondoa katika mbio za kumuwania Mahrez mwezi Januari baada ya Leicester kumzuia kuondoka.

Mahrez amesema aina ya uchezaji wa City inavutia na ni timu ambayo kila mchezaji anatamani kuichezea.

Mahrez amefunga magoli 48 huku 39 yakiwa ni kwenye ligi kuu ya England
”Kuwaona wakicheza limekua jambo la kuvutia sana,” alisema Mahrez.

”Pep Guardiola ni kocha ambaye anapenda soka la kushambulia, na kiwango cha City msimu uliopita kilikua kizuri sana.

Riyad Mahrez kukamilisha uhamisho wake, anaelekea wapi?
”Nafikiri tutafanikiwa zaidi miaka ya mbeleni na ninaamini aina yangu ya uchezaji inaweza kuwa nzuri zaidi chini ya uongozi wa Pep.”

Ni wachezaji wanne pekee waliochangia magoli mengi zaidi ya Mahrez msimu wa 2017-18
Mahrez alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka baada ya Leicester kuwashangaza wengi kwa kuwa mabingwa wa England msimu wa 2015-16 akiondoka klabuni hapo kwa rekodi ya ufungaji wa magoli 48 katika michezo 179.

Leicester inasema ”Alicheza kwa moyo mmoja akiwa karibu sana na amashabiki kwa miaka minne na nusu ndani ya klabu.”

”Kumbukumbu yake itadumu daima katika historia na mioyoni mwa mashabiki”.

Mahrez aliomba kuhama Leicester mwezi Januari lakini ikashindikana baada ya Manchester City kukataa kutoa Paundi milioni 95 iliyokua ikihitajika na Leicester.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *