Home / Habari Za Kitaifa / RAIA WA MAREKANI KORTINI KWA KUSAFIRISHA HEROIN

RAIA WA MAREKANI KORTINI KWA KUSAFIRISHA HEROIN

RAIA wa Marekani ambaye ni mkazi wa Jimbo la Michigan, Lione Rayford, amefi kishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kusafi risha zaidi ya kilo mbili za dawa za kulevya aina ya heroin.

Rayford amefikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Wanjah Hamza. Wakili wa Serikali, Constantine Kakula alidai kuwa mshitakiwa huyo ameshitakiwa chini ya kifungu cha sheria namba 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2017.

Alidai kuwa sheria hiyo inayosomeka pamoja na paragrafu ya 23 ya jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu uchumi, sura ya 200 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 na kufanyiwa marekebisho na Sheria namba 3 ya 2016. Kakula alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) Alidai mshitakiwa alikutwa akisafirisha dawa ya kulevya aina ya heroine yenye uzito wa kilogramu 2.188.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa, mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya isipokuwa Mahakama Kuu au hadi Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) atoe kibali kuruhusu kesi hiyo kuendelea. Hata hivyo, upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hata hivyo, Hakimu Hamza aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 19, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa na mshitakiwa alirudishwa rumande

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *