Home / Habari Za Kitaifa / NEC YAVIBANA VYAMA UCHAGUZI JIMBO LA BUYUNGU

NEC YAVIBANA VYAMA UCHAGUZI JIMBO LA BUYUNGU

KATIKA kukabiliana na vurugu kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Buyungu na udiwani katika kata 79, utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeviagiza vyama vya siasa kuwasilisha majina ya mawakala wa uchaguzi siku saba kabla ya siku ya kupiga kura.

Pia imewaagiza wasimamizi wa uchaguzi katika uchaguzi huo kutoa majina ya mawakala hao watakaokuwa wamependekezwa na vyama vya siasa kwenye vituo husika kabla siku ya kupiga kura ili kuondoa mtafaruku unaoweza kujitokeza kwa kukosekana kwa majina hayo kwa wakati. Agosti 12, utafanyika uchaguzi wa nafasi moja ya ubunge katika Jimbo la Buyungu lililopo Halmashauri ya Kakonko mkoani Kigoma na nafasi 79 za udiwani kwenye kata 79 zinazopatikana kwenye halmashauri 43 ndani ya mikoa 24 ya Tanzania bara.

Katika kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa haki, jana Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage aliongoza kikao cha majadiliano na muongozo kilichoshirikisha viongozi wa vyama vya siasa katika kuujadili uchaguzi huo. Jaji Kaijage alisema, ili kufanikisha uchaguzi huo ufanyike kwa amani, NEC imevitaka vyama vya siasa kuwasilisha majina ya mawakala wao mapema kwa wasimamizi wa uchaguzi ili ifahamike kila wakala na kituo atakachosimamia.

Alivitaka vyama hivyo kuwasilisha majina hayo kwa maandishi kuelezea anuani za mawakala husika. Amebainisha kuwapo kwa changamoto kwenye uwasilishwaji wa majina ya mawakala, hali inayopelekea kuibuka kwa vurugu. “Nimeviagiza vyama vya siasa kutoa majina ya mawakala wao mapema ili wasimamizi wawe na muda wa kutosha wa kuyashughulikia na kuwapeleka kwenye vituo vya kupigia kura mapema zaidi, niwasihi wakuu wa vyama vya siasa kuepuka kuwapeleka mawakala wao moja kwa moja kwenye vituo vya kupigia kura,” alisema Jaji Kaijage.

Pia amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kuzingatia ukomo wa madaraka yao katika kusimamia shughuli za uchaguzi kuanzia kipindi cha kampeni hadi kufikia siku ya kutangazwa kwa matokeo. Aliongeza;“Hakuna aliye juu ya sheria za uchaguzi na kanuni zilizotungwa kusimamia uchaguzi, serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, vyama vya siasa, wagombea na wananchi wa ujumla wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo hii kwa mujibu wa sheria na inapaswa kuzingatiwa.”

Alisema, fomu za uteuzi zitatolewa kuanzia Julai 8 hadi 14 huku uteuzi wa wagombea ukipangwa kufanyika Julai 14 na kampeni za uchaguzi zitaanza Julai 15 kisha kumalizika Agosti 11 ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya uchaguzi ambayo ni Agosti 12. Alibainisha kuwa upande wa watendaji wa uchaguzi katika jimbo la Buyungu kutakuwa na wasimamizi wa uchaguzi 44, wasimamizi wasaidizi ngazi ya jimbo 88 na maofisa uchaguzi 44. Aliongeza wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata ni 184 na kwa upande wa vituo vya kupigia kura kutakuwa na wasimamizi wa vituo 1,601 ambapo kutakuwa na wasimamizi wasaidizi wa vituo, makarani waongozaji, walinzi na mawakala wa vyama vya siasa.

Kinyang’anyiro chashika kasi Katika hatua nyingine kinyang’anyiro cha mbio za ubunge katika jimbo la Buyungu kimezidi kushika kasi baada ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumtangaza mgombea wao huku Chama cha ACT – Wazalendo kikitarajia kumaliza mchakato wa kumtangaza mgombea wao leo.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kigoma, Ally Kisala alisema kuwa Ukawa wamemtangaza Elia Kanjero ambaye ni Diwani wa Kata ya Gwarama kuwa mgombea ubunge. Kisala alisema kuwa mgombea huyo anaungwa mkono na vyama vyote vilivyopo Ukawa na kwamba wanasubiri tarehe ya kuanza kampeni ili kuanza kumnadi.

Nacho Chama cha ACT – Wazalendo kinatarajia kukamilisha mchakato wa kumpata mgombea wao leo huku wakikana kuwemo makubaliano na Ukawa kusimamisha mgombea mmoja. Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Mkoa wa Kigoma, Sendwe Ibrahim aliliambia gazeti hili kwamba Mkutano Mkuu wa Jimbo unatarajia kufanyika leo, lengo likiwa ni kumpata mgombea ubunge wa

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *