Home / Habari Za Kitaifa / ASKARI FFU AJIUA KWA RISASI

ASKARI FFU AJIUA KWA RISASI

ASKARI wa jeshi la Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Michael Hosea amejiua kwa kujipiga risasi shingoni na kutokea utosini mwake.

Kaimu Kamanda wa jeshi hilo mkoani Tabora, Graifton Mushi amesema,tukio hilo lilitokea Julai 10, mwaka huu, 11:45 alfajiri.

Graifton amesema Hosea mwenye namba G.8845 PC alijipiga risasi kwa kutumia silaha aina ya SMG na kufa papo hapo.

Kamanda huyo amesema askari huyo alijiua baada ya kuwasalimia askari wenzake chumba cha kuchukulia silaha tayari kuwahi katika lindo lake la Benki ya Access.

Amesema, baada ya kuchukua silaha katika chumba hicho alitoka kupitia chumba cha walinzi cha kupumzikia kwa ajili ya kwenda foleni ili aingie kazini.

Kamanda Hugo aliendelea kusema kuwa askari huyo alipofika mlango wa kutoka nje alijipiga risasi nne shingoni ambazo zilitokea utosini na akafa papo hapo.

Amesema bado chanzo cha kujiua askari huyo hakijafahamika.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba

HISTORIA YA MAREHEMU ISAAC NYAGABONA MUYENJWA GAMBA. Ratiba Kwa Ufupi Jumatatu Alfajiri – Kupokea Mwili Airport …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *