Home / Michezo / Alex Oxlade-Chamberlain: kiungo wa kati wa kukosa msimu mrefu wa 2018-19

Alex Oxlade-Chamberlain: kiungo wa kati wa kukosa msimu mrefu wa 2018-19


Alex Oxlade-Chamberlain aliichezea Liverpool msimu uliopita na kufunga magoli matano

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza Alex Oxlade-Chamberlain anatarajiwa kukosa kipindi kirefu cha msimu wa 2018-19 kulingana na mkufunzi Jurgen Klopp.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hajacheza tangu alipopata jereha la goti wakati wa mechi ya nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Roma mnamo mwezi Aprili.

Tunahisi sasa ndio wakati mwafaka kuwaambia watu kwamba Ox , msimu huu utakuwa wa kuuguza jeraha, alisema Klopp.

Tulijua hili tangu alipopata jeraha hilo. OX-laide Chamberlain alikosa kombe la dunia baada ya kupata jeraha la goti wakati alipokuwa akimkabili mchezaji wa Roma Aleksandar Kolarov katika uwanja wa Anfield tarehe 24 April.

Akicheza mara 32 , alihamia Liverpool kutoka Arsenal msimu uliopita kwa dau la £35m.

Oxlade-Chamberlain alifanyiwa upasuaji msimu uliopita, lakini Klopp alisema kuwa mchezaji huyo hakutaka ubaya wa jeraha hilo kutajwa wakati huo kwa kuwa ungeathiri kampeni ya kutaka kushinda kombe la vilabu bingwa.

Liverpool ilishindwa 3-1 katika fainali na Real Madrid.

Alex Oxlade-Chamberlainalichapisha picha hii katika mtandao wake wa Instagram

“Hakuna mabadiliko yoyote , kila kitu kimekwenda kulingana na wakati tulioweka”, alisema Klopp. Habari mpya ni kwamba sasa tumeanza kutoa habari kuhusu jeraha hilo hadharani.

”Hatukutaka habari hizi kuathiri mwisho wa msimu, kwa kweli tuliona ni vyema kuzungumza wakati unaofaa”.

About komaji

Naitwa Ramadhani Shabani Komaji , Ni kijana wa Kitanzania mwenye upendondo na Kila Mwanadamu , Amani upendo furaha ndiyo Faraja ya maisha yangu, Tovuti yetu inazungumzia mambo yote ya kijamii na Kiimani mwenye kupenda kuchangia maendeleo na uboreshaji wa Tovuti yetu twamkaribisha sana +255655004100

Check Also

Nyota wa Afrika wamkumbuka mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha

Riyad Mahrez (kushoto) ni mmoja ya walitoa heshima zao kwa Vichai Srivaddhanaprabha Wachezaji wa Kiafrika …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *